Norton Password Manager
ID
admmjipmmciaobhojoghlmleefbicajgHifadhi na tengeneza nywila katika hifadhi ya wingu iliyosimbwa kwa njia fiche, jaza taarifa za kuingia kiotomatiki na usawazishe taarifa za kuingia kwenye vifaa vyote.
Maelezo ya kiendelezi
Picha za skrini
Maelezo
Kidhibiti cha nywila kinachotumia wingu kinachorahisisha kuingia kwenye tovuti unazopenda.
Unataka kidhibiti cha nywila chenye uwezo mkubwa na kisicholipishwa kwa mibofyo michache tu? Norton Password Manager*, inayotolewa na kampuni inayoongoza duniani katika usalama wa watumiaji mtandaoni, hukusaidia kutengeneza, kudhibiti na kuhifadhi nywila imara na za kipekee, na pia kuzisawazisha kwa urahisi kwenye vifaa vyako vyote.¹ Jiunge na mamilioni ya watu wanaoiamini Norton kuwasaidia kurahisisha maisha yao ya kidijitali na kuyalinda zaidi dhidi ya vitisho vya mtandaoni.
Taarifa zako hubaki za faragha hata kwetu kwa sababu husimbwa kwa njia fiche inayozuia hata mtoa huduma kuzisoma kabla ya kuhifadhiwa katika hifadhi yako ya wingu. Unaweza kuongeza usalama wa nywila zako na taarifa nyingine binafsi kwa kuwezesha uthibitishaji kwa vipengele viwili, na pia unaweza kutumia Kufungua Hifadhi Bila Nywila² kufikia hifadhi yako haraka zaidi.
Kutengeneza na kukumbuka nywila changamano si lazima kuwe kugumu. Norton Password Manager hukuruhusu kuingiza nywila zako zilizopo kutoka vyanzo vingine³ na hukusaidia kulinda taarifa zako binafsi kwa kutoa mapendekezo ya kuimarisha nywila, hivyo kuongeza usalama wa maisha yako ya kidijitali mtandaoni.
Kwa nini uchague Norton Password Manager?
💡 Nywila hujazwa kwa mbofyo mmoja
Unapoingia kwenye tovuti, mchakato huwa rahisi zaidi, wa haraka zaidi na unaofaa zaidi. Nywila zako huhifadhiwa katika hifadhi ya mtandaoni, ambayo inaweza kutumika kujaza kiotomatiki taarifa za kuingia mtandaoni kwa mbofyo mmoja.
🔒 Imesimbwa kwa njia fiche
Kwa usimbaji fiche unaozuia hata mtoa huduma kusoma taarifa na uthibitishaji kwa vipengele viwili, ni wewe pekee unayedhibiti ufikiaji wa hifadhi yako ya nywila—hata Norton haiwezi kuifikia. Hatua hizi za usalama husaidia kulinda data yako zaidi dhidi ya wahalifu wa mtandaoni.
💵 Bila malipo*
Norton Password Manager ni ya bila malipo, inapatikana kwa mtu yeyote na inafanya kazi kwenye vifaa vikiwemo kompyuta, tableti na simu.
🔄 Sawazisha nywila¹
Taarifa zako za kuingia na za kadi ya mkopo zinaweza kujazwa kiotomatiki, na pia hifadhi yako yote ya nywila inaweza kusawazishwa ili uweze kuifikia kwenye vifaa vyako vyote.
📱 Kufungua Hifadhi Bila Nywila²
Huhitaji hata kuandika nywila yako kuu. Fikia hifadhi yako haraka zaidi kwa kuidhinisha tu ombi la kuifungua kwenye kifaa chako cha mkononi.
✅ Tathmini ya Nywila
Angalia ikiwa nywila zako ni imara, tengeneza nywila mpya kwa urahisi, au badilisha nywila dhaifu ziwe changamano zaidi.
*Katika toleo la bila malipo la Norton Password Manager, tunahifadhi haki ya kuweka kikomo cha idadi ya vipengee vilivyohifadhiwa (kama vile nywila) wakati wowote. Kikomo hiki hakitaathiri vipengee vyovyote ambavyo tayari vipo kwenye hifadhi yako.
¹ Kifaa chako kinahitaji kuwa kimeunganishwa kwenye Intaneti na kiwe kimewashwa.
² Hufanya kazi kwenye Mac na Windows pekee kupitia kiendelezi kinachotumika, na inahitaji kifaa cha mkononi kilichosakinishwa programu. Lazima uwe umeingia kwenye programu ya Norton Password Manager ya kifaa cha mkononi na kwenye kiendelezi cha kivinjari kwa akaunti ileile, na uwe umesanidi Kufungua Hifadhi Bila Nywila.
³ Hufanya kazi kwenye Mac na Windows pekee kupitia kiendelezi cha kivinjari kinachotumika. Huruhusu kuingiza nywila kutoka kwenye vivinjari na vidhibiti vingine vya nywila, lakini si vivinjari na vidhibiti vyote vya nywila vinavyotumika. Kwa maelezo, nenda: https://support.norton.com/sp/en/us/home/current/solutions/v125566479
SERA YA FARAGHA
Gen inaheshimu faragha ya watumiaji wetu na inalinda data binafsi kwa uangalifu.
Kwa maelezo zaidi: https://www.gendigital.com/privacy
Kwa kutumia programu-jalizi hii, unakubali Makubaliano yetu ya Leseni na Huduma (https://www.gendigital.com/legal/license-services-agreement/) na unathibitisha kuwa umesoma na unatambua Taarifa yetu ya Faragha ya Kimataifa (https://www.gendigital.com/privacy/global-privacy-statement).
Programu-jalizi hii hutumia Google Analytics Measurement Protocol kutuma taarifa kuhusu hitilafu kubwa na matumizi ya vipengele kwenye huduma za Google Analytics. Gen Digital hutumia huduma za Google Analytics kudumisha na kuboresha programu-jalizi hii, lakini huduma hizo haziendeshwi na Gen Digital.
Ikiwa hukubaliani na ukusanyaji na matumizi haya ya data, tafadhali usisakinishe programu-jalizi hii, au iondoe ikiwa tayari imesakinishwa.
Programu-jalizi hii huweka vigezo vinavyotolewa na Google ili kuficha anwani yako ya IP wakati wa uchakataji wa Google Analytics. Tazama maelezo hapa kuhusu wajibu wetu unaohusiana na matumizi ya Google Analytics, desturi za faragha za Google, na usaidizi wa Google wa kuficha anwani za IP:
- https://developers.google.com/analytics/policy
- https://support.google.com/analytics/answer/6004245
- https://support.google.com/analytics/answer/2763052
Hakimiliki © 1997 – 2026 Gen Digital Inc. Haki zote zimehifadhiwa.
Alama zote za biashara, alama za huduma na majina ya biashara (kwa pamoja, “Alama”) ni alama za biashara au alama za biashara zilizosajiliwa za Gen Digital Inc. au kampuni zake shirikishi (“Gen”), au za wamiliki wengine husika ambao wameipa Gen haki ya kutumia Alama hizo. Kwa orodha ya Alama za Gen, tafadhali tazama GenDigital.com/trademarks.