Pop up blocker for Chrome™ - Poper Blocker
ID
bkkbcggnhapdmkeljlodobbkopceicheZuia madirisha ibukizi, matangazo, mabango ya vidakuzi na arifa, yakiwemo matangazo ya video kwenye YouTube; jaribio la bure la siku 7 linatolewa.
Picha za skrini
Maelezo
Zuia madirisha ibukizi, matangazo, maombi ya vidakuzi, vifuatiliaji, arifa, matangazo kwenye mitandao ya kijamii na zaidi. Anza kuvinjari bila usumbufu leo.
Ukiwa na Poper Blocker, utafurahia kuvinjari kwa utulivu na bila kukengeushwa kwa kuzuia kiotomatiki madirisha ibukizi yasiyotakikana, matangazo yanayoingilia shughuli zako, mabango ya kuomba ruhusa ya vidakuzi, arifa za tovuti, matangazo kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii, matangazo ya video kwenye Youtube, na mengi zaidi! Poper Blocker ndiyo suluhisho bora kabisa la kuzuia madirisha ibukizi na kuondoa matangazo kwenye Chrome. Zuia matangazo ya video kwenye tovuti kama Crunchyroll na Dailymotion.
Fahamu vipengele vyetu muhimu:
🛑 Zuia aina zote za madirisha ibukizi kwenye tovuti yoyote:
Sasa unaweza kuzuia kabisa aina yoyote ya tangazo ibukizi, dirisha ibukizi au kichupo kipya bila kujali aina ya tovuti unayovinjari. Poper itakumbuka kilichozuiwa ili dirisha ibukizi liendelee kuzuiwa na lisionekane. Furahia kuvinjari bila usumbufu ukitumia kizuia matangazo hiki cha hali ya juu.
📰 Kuzuia matangazo kwenye tovuti yoyote:
Furahia kuvinjari intaneti kwa kuficha kiotomatiki matangazo yasiyoisha kwenye tovuti yoyote. Haya yanajumuisha matangazo ya mabango, matangazo ya maandishi na matangazo mengine yanayokera. Poper Blocker hufanya kazi kama kichujio chenye nguvu cha maudhui ili kukuwezesha kuvinjari kwa kasi.
▶️ Ficha matangazo kwenye video za YouTube:
Furahia video na muziki kwenye YouTube bila matangazo yanayokera yanayoonyeshwa kabla ya video, katikati ya video au matangazo ya video ambayo huwezi kuyaruka. Kizuia matangazo chetu cha YouTube huhakikisha unatazama bila kukatizwa kabisa.
🎬 Kizuia matangazo wakati wa kutiririsha video:
Furahia utiririshaji laini zaidi na usio na usumbufu kwenye majukwaa unayopenda ya video. Poper Blocker huondoa matangazo yanayokatiza kwenye tovuti kama Dailymotion, Crunchyroll, Tubi na nyingine nyingi, na kukuwezesha kuanza moja kwa moja kutazama maudhui unayotaka. Uwezo wa kuzuia matangazo ya Twitch pia unakuja, ili uwe na udhibiti mkubwa zaidi wa utiririshaji wako.
👤 Ondoa matangazo na maudhui yaliyofadhiliwa kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii:
Furahia kuvinjari bila kukengeushwa kwenye Facebook, Instagram, LinkedIn na X (zamani Twitter), bila matangazo yoyote yanayokatiza na kujaza mlisho wako. Zingatia maudhui yaliyo muhimu kwako kwa kutumia kipengele chetu kilichojumuishwa cha kuzuia matangazo kwenye mitandao ya kijamii.
Zaidi - Kichujio cha Maudhui ya Mitandao ya Kijamii:
Dhibiti mlisho wako kwenye Facebook, Linkedin, Instagram na X (Twitter) kwa kuficha machapisho yenye neno lolote mahususi unalochagua. Hii inakupa udhibiti kamili wa maudhui yako mtandaoni.
🍪 Ficha maombi ya idhini ya vidakuzi na ujumbe ili visionekane unapovinjari:
Kwa nini tovuti nyingi zinataka tuache tunachofanya ili kutazama mabango yao ya GDPR au arifa za vidakuzi? Ondoa mabango na ujumbe huu unaoingilia shughuli zako ili uweze kuvinjari bila kukatizwa.
🗑️ Ondoa madirisha ibukizi ya hali ya juu (tabaka zinazofunika ukurasa) yanayoficha maudhui na kurasa unazotazama:
Tabaka zinazofunika ukurasa ni vizuizi vinavyokatiza shughuli zako kwa kuweka picha juu ya ukurasa wa wavuti unaovinjari. Vizuia maudhui vingi havizuii tabaka hizi, lakini Poper Blocker huzizuia. Hii inajumuisha tabaka zinazofunika skrini nzima na madirisha yanayokulazimisha kuyashughulikia kabla ya kuendelea.
❗ Zuia arifa za tovuti zinazokuvuruga:
Arifa za tovuti zinazoendelea kujitokeza kwenye tovuti unayotembelea hukengeusha na si za lazima. Poper itazuia kiotomatiki arifa zote za kivinjari na arifa zinazotumwa moja kwa moja, na kukusaidia kuzingatia vizuri zaidi.
🖱️ Ficha kipengele chochote cha kiolesura cha wavuti unachotaka kwa kubofya tu:
Ficha vipengele vya wavuti na vitufe visivyohitajika, na ubinafsishe kuvinjari kwako kwa kila mbofyo. Hii hukuwezesha kuvinjari kwa namna unayopenda na hufanya kazi kama zana rahisi ya kuondoa vipengele vya ukurasa.
📖 Tazama maudhui yaliyozuiwa na historia ya shughuli ili kuelewa kinachozuiwa na wapi:
Rejelea historia yako ya Poper Blocker ili kuona kilichozuiwa. Unaweza kufanya mabadiliko kwenye maudhui yako yaliyozuiwa na historia ya shughuli wakati wowote. Kipengele hiki huleta uwazi na hukusaidia kudhibiti ruhusa za tovuti zako.
✔️ Unda orodha ya tovuti zinazoruhusiwa kuonyesha madirisha ibukizi:
Fanya mabadiliko wakati wowote kwenye orodha yako ya tovuti zilizoidhinishwa. Hii hukupa uhuru wa kuchagua na huhakikisha programu yetu ya kuzuia matangazo haiingiliani na tovuti unazoamini au kuunga mkono.
Poper Blocker ni kiendelezi cha Chrome chenye kusudi moja la kuzuia matangazo, ambacho huzuia aina zote za madirisha ibukizi na matangazo kwenye tovuti yoyote na tovuti zote. Unapotiririsha kipindi au mchezo unaoupenda, kuvinjari maudhui ya watu wazima au kusoma habari, Poper Blocker hufanya kazi chinichini ili kuzuia madirisha yote ibukizi ya matangazo na hukuarifu dirisha ibukizi linapozuiwa. Hii huhakikisha kuvinjari bila kukengeushwa na pia husaidia kudumisha uwezo mkubwa unaopatikana wa CPU, hivyo kuwezesha utendaji na ufanyaji kazi ulio laini zaidi.
Pakua Poper Blocker leo ili upate uzuiaji bora zaidi wa matangazo na udhibiti wa madirisha ibukizi.
Uko tayari kukomesha madirisha ibukizi, matangazo, tabaka zinazofunika kurasa na arifa zinazoingilia shughuli zako? Jisajili leo ufurahie jaribio la BURE la siku 7 na uone jinsi intaneti isiyo na matangazo inavyopaswa kuwa.
💡 Teknolojia na Faragha
Teknolojia yetu:
Kwa msaada wa wateja wetu, tunaweza kutambua tovuti zote zinazoonyesha madirisha ibukizi, tabaka zinazofunika kurasa na madirisha yanayofunguka nyuma ya dirisha kuu. Kila URL inayotembelewa hukaguliwa kwa kulinganishwa na hifadhidata yetu na kusajiliwa humo ili kutambua suluhisho la uzuiaji linalohitajika. Poper Blocker pia hupokea na kuchanganua data husika kuhusu tovuti zilizotembelewa.
Ili kuzuia madirisha yote ibukizi kwa ufanisi, tutahitaji ruhusa yako ya kufikia taarifa hizi.
Utapata kila kitu kingine unachohitaji kujua katika Sera yetu ya Faragha:
https://poperblocker.com/privacy/