Picha za skrini

Maelezo

Huonyesha jinsi API ya chrome.fontSettings inavyofanya kazi kwa kuruhusu watumiaji kubadilisha mtindo wa fonti zinazoonekana kwenye kurasa za wavuti. Kiendelezi hiki hukuwezesha kubinafsisha mipangilio ya fonti kwa mifumo mbalimbali ya uandishi. Kwa mfano, unaweza kuweka fonti chaguomsingi ya maudhui ya Kichina Kilichorahisishwa iwe tofauti na fonti ya maudhui ya Kijapani. Mipangilio ni ya kila mfumo wa uandishi kama ulivyobainishwa katika ISO 15924, si ya kila lugha. Kwa mfano, kuna mpangilio mmoja wa maandishi ya Kisiriliki badala ya mipangilio tofauti ya Kirusi, Kiukraini na kadhalika. Chrome itatumia mipangilio ya fonti inayodhibitiwa na kiendelezi hiki ikiwa masharti YOTE MAWILI yafuatayo yametimizwa: 1) Ukurasa wa wavuti umetangaza lugha ya maudhui, kwa mfano kwa kutumia sifa ya HTML lang; na 2) Ukurasa wa wavuti haujabainisha fonti ya kutumia. Ili kutumia kiendelezi hiki, kiongeze kwenye Chrome, kisha nenda kwenye chrome://extensions na ubofye kiungo cha “Chaguo” cha kiendelezi hiki.