Google Scholar PDF Reader
ID
dahenjhkoodjbpjheillcadbppiidmhpSoma PDF za utafiti ukiwa na mwonekano wa awali wa marejeleo, mihtasari ya AI, uangaziaji na nukuu, na uhifadhi makala kwenye maktaba yako ya Scholar.
Picha za skrini
Maelezo
Boresha usomaji wako wa makala za utafiti: fuata marejeleo, pitia muhtasari haraka, nenda moja kwa moja kwenye vielelezo, nukuu na uhifadhi.
Unaposakinisha Scholar Reader, PDF kwenye tovuti zote zitakuwa na mwonekano mpya katika Chrome. Ili kuwezesha hili, Chrome itaomba ruhusa za kusoma na kubadilisha data kwenye tovuti zote. Scholar Reader haibadilishi chochote isipokuwa jinsi PDF zinavyoonyeshwa.
• Tazama mwonekano wa awali wa marejeleo unaposoma. Bofya nukuu iliyo ndani ya maandishi ili kuona muhtasari na kupata PDF.
• Soma haraka zaidi kwa muhtasari wa AI. Pata picha ya jumla kwa haraka na ubofye vipengele vya kuvutia vya orodha ili kwenda moja kwa moja kwenye sehemu husika ndani ya makala.
• Angazia maandishi na uongeze maoni kwenye PDF. Maandishi yaliyoangaziwa huhifadhiwa kwenye maktaba yako ya Scholar.
• Rekebisha mwonekano ili ufae macho yako kwa hali za mwanga, giza na usiku.
• Nakili na ubandike miundo ya kawaida ya nukuu bila kuondoka kwenye makala.
• Hifadhi makala kwenye maktaba yako ya Scholar ili uzisome au kuzinukuu baadaye.
• Bofya mahali ambapo kielelezo kimetajwa ndani ya maandishi ili kukiona, kisha ubofye kitufe cha kurudi ili kuendelea kusoma.
Kwa kusakinisha kiendelezi hiki, unakubali Sheria na Masharti ya Google na Sera ya Faragha katika https://www.google.com/intl/en/policies/.