Picha za skrini

Maelezo

Zana maridadi na yenye ufanisi zaidi ya kuongeza maelezo. Piga picha au rekodi ukurasa wako wa wavuti au skrini ya kompyuta. Ongeza maelezo kwenye picha ya skrini ya ukurasa wako wa wavuti au kwenye picha za kompyuta yako, kama vile sampuli za usanifu, michoro na vielelezo, kwa kupakia picha husika. Angalia vipengele vilivyo hapa chini. KUPIGA PICHA YA SKRINI - Piga picha ya ukurasa mzima, eneo linaloonekana au sehemu tu ya ukurasa. - Piga picha ya skrini nzima ya kompyuta au dirisha la programu. - Tumia upigaji uliocheleweshwa kupiga picha ya sehemu zinazoonekana tu baada ya kubofya kiungo au kitufe kwenye ukurasa. KIREKODI CHA SKRINI - Rekodi skrini inayoonekana ya ukurasa au sehemu ya ukurasa. - Rekodi skrini nzima ya kompyuta au dirisha la programu. KIREKODI CHA VIDEO - Rekodi video kwa kamera yako ya wavuti ili kushiriki maarifa yako na hadhira unayolenga. MAELEZO KWENYE PICHA - Tumia maumbo ya mraba na duara kuweka alama kwenye maeneo ya kutolea maoni. - Zana ya kuchora kwa mkono hukuwezesha kuzungushia sehemu kwa usahihi bila kuathiri sehemu nyingine za hati. - Kalamu ya kuangazia husisitiza maudhui yanayohitaji kuangaliwa. - Ongeza maoni yanayohusiana na muktadha kwenye maeneo yaliyoangaziwa. - Tumia zana za kuweka lebo kuhesabu maeneo ya kutolea maoni na kuyaelezea katika programu yoyote ya mawasiliano baada ya kumaliza. - Tia ukungu au futa kwa kupaka data ya faragha au ya siri. KUSHIRIKI NA KUPAKIA KWENYE WINGU - Pata kiungo kinachoweza kushirikiwa na ukishiriki kwenye mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter na WhatsApp) na tovuti/programu nyingine. - Pakia faili kwenye akaunti zako za Zoho WorkDrive, Google Drive, OneDrive na Dropbox. - Shiriki faili katika Zoho Cliq, Zoho Connect, Zoho Projects na Zoho Sprints. MAPENDEKEZO Badilisha thamani chaguomsingi kama rangi ya mstari, familia ya fonti na rangi ya maandishi kulingana na unavyopenda. MSAADA Kwa maswali au msaada, tuma barua pepe kwa [email protected].