Britannica School Insights
ID
ecimfebadcfiablhgjpheinknpdkdjhhOnyesha maudhui yanayofaa ya Britannica School kando ya matokeo ya Google ya lugha ya Kiingereza kwa walio na usajili wa Britannica School.
Maelezo ya kiendelezi
Picha za skrini
Maelezo
Je, una usajili wa Britannica School?
Boresha matumizi yako ya utafutaji wa Google kwa kuongeza maudhui ya Britannica School moja kwa moja kwenye matokeo yako ya utafutaji wa wavuti.
Kiendelezi cha kivinjari cha bure cha Britannica School, Britannica School Insights, kinabadilisha jinsi wanafunzi na shule wanavyogundua taarifa mpya kwa kuleta taarifa zilizohakikiwa upande wa kulia wa kurasa za matokeo ya utafutaji wa Google.
Kiendelezi hiki huonyesha taarifa zilizothibitishwa na Britannica na njia za kuchunguza zinazofichua uhusiano wa kipekee, maarifa yasiyo ya kawaida, muktadha na mitazamo kuhusu mada zinazotafutwa kwa lugha ya Kiingereza.
-Chuja taarifa nyingi zisizo na umuhimu kwenye Intaneti ili kufanya utafiti kwa njia bora zaidi.
-Jenga ujuzi wa kutumia taarifa za kidijitali kwa kuhakikisha kuwa chanzo kilichohakikiwa kinaonekana pamoja na matokeo ya kawaida ya utafutaji.
-Pata ukweli kwa haraka au chunguza kwa kina zaidi muktadha na uhusiano kuhusu mada unazotafuta.
-Amini kwamba kiendelezi hiki kitaonyesha tu matokeo ya utafutaji yenye uhusiano wa karibu sana na unachotafuta.
___________________________________________________________________________________
S: Nitaanzaje kutumia Britannica School Insights?
Ikiwa una usajili wa Britannica School, bofya “Ongeza kwenye Chrome” na uendelee kutafuta kama kawaida. Britannica inapokuwa na matokeo yanayohusiana kwa karibu sana na unachotafuta, yataonekana upande wa kulia wa ukurasa wako wa utafutaji. Ikiwa huna usajili wa Britannica School, tafadhali tembelea Britannica School - Britannica Education - US ili ujifunze zaidi kuhusu usajili.
S: Je, Britannica School Insights itabadilisha kinachoonekana katika matokeo yangu ya utafutaji? Ninaweza kuona vyanzo gani?
Matokeo yako ya utafutaji yanabaki yaleyale, na bado utaweza kuona nyenzo zote ulizoweza kuona hapo awali. Britannica School Insights huonyesha matokeo ya ziada upande wa kulia wa ukurasa wako wa utafutaji, kutoka kwenye kiwango cha shule ya sekondari cha Britannica School, kunapokuwa na maudhui yanayofaa ya kushiriki.
S: Nilijaribu kutafuta taarifa kwenye Google. Kwa nini Britannica School Insights haikuonekana?
Insights itaonekana tu wakati Britannica ina matokeo yanayofaa ya kuonyesha. Wakati Britannica haina taarifa kuhusu mada hiyo, kiendelezi hakitaonekana. Hii husaidia kuweka matokeo yako ya utafutaji wazi na yenye uhusiano na unachotafuta kadiri iwezekanavyo.
S: Britannica School Insights inawezaje kuonyesha muktadha, uhusiano na mitazamo?
Britannica School Insights hutumia teknolojia ya hali ya juu inayomilikiwa na Encyclopaedia Britannica ya kubainisha uhusiano ili kuonyesha maarifa yasiyo ya kawaida na uhusiano wa kipekee.
S: Je, mnafuatilia data yangu au historia yangu ya utafutaji?
Britannica School Insights haishughulikii wala kukusanya taarifa zozote za kibinafsi au nyeti, wala haifuatilii data ya utafutaji. Ikiwa ungependa maelezo zaidi kuhusu sera za kampuni yetu mama, Encyclopaedia Britannica, Inc., tafadhali soma Sera yetu ya Faragha: https://corporate.britannica.com/privacy.html