Picha za skrini

Maelezo

Huiagiza JavaScript ya Google Analytics isitume taarifa kwa Google Analytics. Ili kuwapa wageni wa tovuti uwezo wa kuzuia data zao zisikusanywe na kutumiwa na Google Analytics, tumetengeneza kiendelezi cha kivinjari cha kujiondoa kwenye Google Analytics kwa JavaScript ya Google Analytics (ga.js, analytics.js, dc.js). Ukitaka kujiondoa, pakua na usakinishe kiendelezi kwenye kivinjari chako cha wavuti. Ili kifanye kazi, kiendelezi cha kujiondoa lazima kiweze kupakiwa na kutekelezwa ipasavyo kwenye kivinjari chako. Masasisho ya kivinjari au mfumo wako wa uendeshaji yanaweza kuathiri utendaji wa kiendelezi cha kujiondoa. Maelezo zaidi kuhusu kudhibiti viendelezi vyako vya Chrome yanapatikana kwenye https://support.google.com/chrome/answer/187443?hl=en. Kwa kusakinisha kiendelezi hiki, unakubali Sheria na Masharti ya Chrome Web Store yaliyo kwenye https://ssl.gstatic.com/chrome/webstore/intl/en/gallery_tos.html na Sheria na Masharti ya Google Analytics Opt-out Browser Add-on yaliyo kwenye https://tools.google.com/dlpage/gaoptout/intl/en/eula_text.html.