Picha za skrini

Maelezo

Kiendelezi cha Coinbase Wallet ndiyo njia salama zaidi na rahisi zaidi ya kutumia programu za sarafu za kidijitali katika kivinjari chako. Ulimwengu wa sarafu za kidijitali ndio kwanza unaanza, na Coinbase Wallet ndiyo ufunguo wako wa yale yanayokuja. Coinbase Wallet ni pochi ya sarafu za kidijitali ambayo funguo zake unazihifadhi mwenyewe, inayokupa udhibiti na kukufungulia ulimwengu mzima wa sarafu za kidijitali. Kiendelezi chetu cha kivinjari kinakupa ufikiaji wa ulimwengu wa kusisimua wa huduma za kifedha zilizogatuliwa, NFT na programu zilizogatuliwa – vyote vikiwa karibu nawe. Ukiwa na kiendelezi cha Coinbase Wallet unaweza: - Kuchunguza wavuti iliyogatuliwa kwa kujiamini. - Kuanza mkusanyiko wako wa NFT - Kutumia uwezo wa DeFi kupata mapato - Kufanya biashara ya maelfu ya tokeni kwenye masoko ya kubadilishana yaliyogatuliwa - Kufanya mengi zaidi kwa sarafu zako za kidijitali Kiendelezi cha Coinbase Wallet hukuwezesha kufikia web3 na kuunganisha kwenye maelfu ya programu zilizogatuliwa kwenye Ethereum na mitandao yote inayooana na EVM, ikiwemo Avalanche, Polygon, BNB Chain na mingine. Kiendelezi cha Coinbase Wallet pia kinawezesha kutuma na kupokea Solana na tokeni za SPL. Pata maelezo zaidi kwenye coinbase.com/wallet