Picha za skrini

Maelezo

Pixlr Editor ni kihariri cha picha kwenye kivinjari kwa mahitaji yako yote ya uhariri. Dhibiti picha zako kikamilifu, ikiwemo tabaka na madoido. Pixlr Editor ndicho kihariri cha picha cha mtandaoni chenye uwezo wa hali ya juu kinachopendwa zaidi. Huhitaji kupakua chochote, na ni bure kwa 100%. Ikiwa umezoea kufanya kazi na Gimp, PaintShop Pro au Photoshop, utajisikia umekizoea kihariri hiki cha picha cha mtandaoni. Kina vipengele vingi ambavyo kwa kawaida unaviona katika programu za usanifu wa picha za kompyutani. Anza kutumia zana hii mara moja bila kuhitaji kujisajili. • Huhitaji akaunti. Fungua akaunti ili kupata nafasi ya kuhifadhi bila malipo ukipenda. • Hakuna kitu maalumu cha kupakua au kusakinisha. Kifungue tu kwenye kivinjari chako unapokihitaji. • Hutoa zana kama vile tabaka, zana ya kuchagua eneo kwa kuchora mpaka, vidhibiti vya brashi, kunakili sehemu za picha na vichujio. • Pixlr Library ya faragha ya hiari ambamo unaweza kuhifadhi picha zako zote, zikiwemo picha za kamera. Zana zinajumuisha kupunguza wekundu wa macho, zana ya kuondoa madoa, zana za kuchora, zana za kunakili sehemu za picha, kuongeza ukali wa picha, kutia ukungu na nyingine nyingi. Vichujio vinajumuisha kuiga HDR, mng'ao wa kuvutia, athari ya tilt-shift, ukungu wa Gaussian, kutia kivuli pembezoni, chembechembe kwenye picha na vingine vingi. Marekebisho yanajumuisha mbinu za hali ya juu kama vile viwango, mikunjo, athari ya kuosha filamu kwa kemikali za aina nyingine, kuondoa rangi, viwango vya kiotomatiki, aina ya rangi/ukolezi wa rangi na mwangaza/utofautishaji.