Picha za skrini
Maelezo
Hifadhi vitu unavyotaka kuvirudia baadaye.
HUNA MUDA? HAKUNA TATIZO
Umeona video ya kuchekesha, mazoezi, mapishi au makala unayotaka kutazama au kushiriki na marafiki au familia, lakini huna muda? Kiendelezi cha Chrome cha Save to Facebook hukuwezesha kuhifadhi mambo hayo yote ya kuvutia unayoona kwenye intaneti na kuyapata kwa urahisi baadaye.
PANGA VIZURI
Unapohifadhi kipengee kutoka intaneti kwenye Facebook, tunakusaidia kukipanga kwa kukupa chaguo za mikusanyiko. Ongeza kipengee kwenye mkusanyiko uliopo au uunde mpya—kitakuwa rahisi kukipata ukiwa tayari kukiona au kukishiriki baadaye. Unaweza kuunda mikusanyiko mingi kadiri unavyotaka na kuipa majina yoyote unayotaka.
KWA AJILI YAKO PEKE YAKO (hadi utakapokishiriki)
Ni wewe pekee unayeweza kuona na kufikia vipengee ulivyohifadhi, ambavyo vinawekwa kwenye orodha yako binafsi ya faragha ya Vipengee Vilivyohifadhiwa. Kutoka hapo unaweza kuvishiriki kwenye ratiba yako ya matukio, kwenye kikundi au mahali pengine kwenye Facebook. Kwa kipengele cha Mikusanyiko Inayoshirikiwa, unaweza pia kushiriki mkusanyiko mzima wa vipengee vilivyohifadhiwa na marafiki unaowachagua.
ONA ULICHOHIFADHI KUTOKA POPOTE
Unaweza kufikia haraka vipengee na mikusanyiko uliyohifadhi kwenye Facebook, bila kujali kivinjari chako kinakupeleka wapi. Bofya aikoni ya Save to Facebook, kisha kiungo cha “Ona Vyote” kwenye kona ya juu kulia, na orodha yako ya vilivyohifadhiwa itafunguka katika dirisha tofauti.
Wakati ujao unapopata maudhui ya kuvutia wakati usiofaa, tumia tu kiendelezi cha Save to Facebook. Ukiwa tayari kuyaona, chagua “Vilivyohifadhiwa na Mikusanyiko” kwenye menyu iliyo kushoto mwa Mlisho wa Habari wa Facebook, au andika www.facebook.com/saved kwenye kivinjari.
Jifunze zaidi kuhusu vilivyohifadhiwa na mikusanyiko kwenye Facebook katika https://www.facebook.com/help/516581611792218?helpref=related.
Kwa kutumia kipengele hiki, unakubali Sera ya Data na masharti ya huduma ya Facebook, yanayopatikana katika https://www.facebook.com/legal/terms na https://www.facebook.com/about/privacy