Grammarly: AI Writing Assistant and Grammar Checker App
ID
kbfnbcaeplbcioakkpcpgfkobkghlhenKagua sarufi na uboreshe uandishi kwa mapendekezo ya AI kuhusu uwazi na mtindo wa kujieleza katika Gmail, Google Docs na tovuti nyingine.
Maelezo ya kiendelezi
Picha za skrini
Maelezo
Grammarly ya Chrome hukusaidia kuandika kwa kujiamini. Pata msaada wa AI kuhusu sarufi, uwazi na mtindo wa kujieleza, kuanzia rasimu ya kwanza hadi uhariri wa mwisho.
Grammarly ya Chrome ni mshirika wako wa AI anayepatikana wakati wote ili kukusaidia kuwasiliana kwa uwazi zaidi na kwa namna inayovutia zaidi. Kuanzia kutafuta mawazo hadi uhariri wa mwisho, AI ya hali ya juu ya Grammarly hukusaidia kuandika haraka zaidi na kwa kujiamini zaidi. Inafanya kazi katika kila unachoandika, iwe ni barua pepe, kazi ya shule au pendekezo la biashara.
Msaada wa AI wa hali ya juu unaoweza kuutegemea:
• Tengeneza rasimu kwa mbofyo mmoja ili kukusaidia kuanza haraka zaidi
• Unda mihtasari ili kupanga mawazo kwa uwazi
• Andika upya sentensi ili ziwe na mtiririko mzuri, ziwe wazi na ziwavutie wasomaji
• Rekebisha mtindo wa kujieleza na uchaguzi wa maneno ili vilingane na hadhira yoyote
• Kagua uhalisi kwa kutumia kipengele kilichojumuishwa cha kutambua wizi wa maandishi na hatua za ulinzi zinazohusu maudhui ya AI
Na sasa, kwa Superhuman Go, unaweza kufanya zaidi ya kuandika. Go hufanya kazi pamoja nawe katika Chrome ili kurahisisha kazi na kupunguza kukatizwa—ikiunganisha msaada wa AI wa Grammarly unaoaminika katika uandishi na zana zinazokusaidia kudumisha umakini na kufanya kazi kwa ufanisi. Kwa sasa Go inapatikana kama toleo la beta unalochagua kujiunga nalo, na unaweza kuiwezesha moja kwa moja katika mipangilio ya kiendelezi chako cha Chrome.
➤ Jinsi inavyofanya kazi
Grammarly huunganishwa moja kwa moja na kivinjari chako, ikitoa mapendekezo papo hapo unapoandika katika Gmail, Google Docs, LinkedIn na tovuti nyingine zaidi ya 500,000.
• Ona masahihisho na maboresho papo hapo
• Panua maelezo ya marekebisho ili kujua “kwa nini” yamependekezwa na kuimarisha ujuzi wako
• Dumisha umakini kwa kutumia Go, msaidizi wa AI anayeelewa unachofanyia kazi na kukupa msaada mapema bila kusubiri uombe
➤ Ni nini kimejumuishwa?
Free – Zana muhimu za kuandika kwa kujiamini:
• Masahihisho ya sarufi, tahajia na uakifishaji
• Mapendekezo ya kuboresha uwazi na mtindo wa kujieleza
• Uwekaji wa marejeleo kiotomatiki kwa mitindo ya APA, MLA na Chicago
• Msaada wa AI wa kutafuta mawazo, kuandika rasimu na kuandika upya
Pro – Kila kilicho katika Free, pamoja na:
• Uandishi upya wa sentensi ili ziwe wazi, ziwe na mtiririko mzuri na ziwavutie wasomaji
• Maboresho ya mtindo wa kujieleza, kiwango cha urasmi na uchaguzi wa maneno
• Taarifa kuhusu hadhira zinazokusaidia kuelekeza jinsi ujumbe wako unavyopokelewa
• Maoni yaliyolengwa kwa kazi za kitaaluma, kiufundi au kikazi
• Utambuzi wa wizi wa maandishi na ukaguzi wa maudhui ya AI
• Vipengele vya timu kama vile miongozo ya mtindo wa uandishi na wasifu wa mitindo ya kujieleza (kwa watumiaji wa biashara)
➤ Inaaminiwa na mamilioni ya watu
“Grammarly inajieleza kwa haki kuwa zaidi ya kikagua tahajia cha kawaida ... Grammarly ina zana ya AI zalishi inayokusaidia kuunda mihtasari, kutafuta mawazo na hata kutengeneza maandishi.” —CNET
“Mapendekezo ya AI ya hali ya juu ya Grammarly yanafanya zaidi ya kuonyesha tu makosa ya sarufi: yanatoa mapendekezo mahiri ya kuboresha uwazi, mtindo wa kujieleza na ufupi wa chochote unachoandika.” —Tom’s Guide
“Uzuri wa zana hii ni kwamba hutumia AI kuonyesha mifano ya jinsi kazi yako inavyoweza kuboreshwa badala ya kukufanyia maboresho hayo.” —ZDNet
➤ Njia nyingine za kutumia Grammarly
• Programu ya kompyuta: Tumia Grammarly katika Word, Outlook, Slack na programu nyingine kwa kupakua Grammarly kwenye kompyuta yako → www.grammarly.com/desktop
• Docs: Eneo maalumu la kuandikia la Grammarly kwa umakini wa kina na maarifa ya kimkakati → www.grammarly.com/docs
➤ Faragha na usalama unaoweza kuamini
Faragha na usalama wa data yako ni msingi wa kila tunachofanya. Pata maelezo zaidi kuhusu mbinu yetu ya uaminifu na usalama inayoweka watumiaji mbele: www.grammarly.com/trust
Wakazi wa California, tafadhali angalieni Taarifa ya Faragha ya California: https://www.grammarly.com/privacy-policy#sectionSingleColumn_47y4NWiOf89wt12wcc6a74
Kwa kusakinisha kiendelezi, unakubali na kuthibitisha kuwa umefahamu yafuatayo:
www.grammarly.com/terms
www.grammarly.com/privacy-policy