Picha za skrini

Maelezo

Kiendelezi cha Tag Assistant hufanya kazi pamoja na Tag Assistant ili kusaidia kutatua matatizo ya usakinishaji wa gtag.js na Google Tag Manager. Tunashukuru kwa maoni yako—tumeyasikiliza na tutasasisha na kurudisha uwezo wa kutatua hitilafu moja kwa moja kwenye ukurasa. Vipengele vingine vya kusisimua vinakuja. Tag Assistant hukusaidia kusakinisha na kutatua matatizo ya tagi zako za Google, zikiwemo Google Analytics, Google Ads, Tag Manager na nyinginezo. Unapokibofya, kiendelezi huonyesha tagi za Google zinazopatikana kwenye ukurasa katika kidirisha cha pembeni. Nenda tu kwenye ukurasa wowote, na Tag Assistant itakuambia ni tagi zipi zilizopo. Tutaongeza vipengele zaidi vya uchunguzi wa matatizo hivi karibuni. Kitufe cha “Tatua matatizo” huwasha hali yetu ya kutatua hitilafu kupitia tagassistant.google.com. Zana hii ya hali ya juu hukuwezesha kutatua hitilafu kwenye tovuti yako, ikiwa ni pamoja na iframe, ndani ya kipindi kimoja. Hutoa uchunguzi wa kina ili kukusaidia kuthibitisha, kutambua matatizo na kuyatatua katika utekelezaji wako. Data ya kipindi inapatikana kwa ukaguzi kwenye tagassistant.google.com. INAKUJA HIVI KARIBUNI: Mwongozo wa hatua kwa hatua wa kusakinisha tagi kwenye zana maarufu za kutengeneza tovuti. Kwa kusakinisha kiendelezi hiki, unakubali Sheria na Masharti ya Google pamoja na Sera yake ya Faragha zinazopatikana kwenye https://www.google.com/intl/en/policies/.