Picha za skrini

Maelezo

Hukulinda dhidi ya ufuatiliaji kupitia usambazaji wa maudhui wa kati wa “bure”. Huzuia maombi mengi kufikia mitandao kama Google Hosted Libraries, na hutoa faili za ndani ili kuzuia tovuti kuharibika utendaji. Hukamilisha vizuiaji vya kawaida vya maudhui. ---------------------------------------------------------------- Tovuti zimeanza kutegemea zaidi na zaidi wahusika wengine wakubwa kwa usambazaji wa maudhui. Kughairi maombi ya matangazo au vifuatiliaji kwa kawaida hakusababishi matatizo, lakini kuzuia maudhui halisi, kama inavyotarajiwa, huharibu utendaji wa kurasa. Lengo la kiongezi hiki ni kuondoa mpatanishi kwa kutoa faili za ndani (zilizojumuishwa) kwa kasi ya umeme ili kuboresha faragha mtandaoni. • Hulinda faragha kwa kuepuka mitandao mikubwa ya usambazaji inayodai kutoa huduma za bure. • Hukamilisha vizuiaji vya kawaida kama uBlock Origin (inapendekezwa), Adblock Plus, na vingine. • Hufanya kazi mara tu baada ya kusakinishwa; haihitaji kabisa usanidi wowote wa awali. Kumbuka: Decentraleyes si suluhisho la kimiujiza kwa kila tatizo, lakini huzuia tovuti nyingi kukufanya utume maombi ya aina hizi. Pia unaweza kuweka Decentraleyes izuie maombi ya rasilimali zozote za CDN zinazokosekana.