Microsoft Power Automate
ID
ljglajjnnkapghbckkcmodicjhacbfhkOtomatisha fomu za wavuti, uchimbaji wa data na kazi nyingine za kivinjari kwa kutumia Power Automate ya kompyuta, toleo la 2.27 au la baadaye.
Maelezo ya kiendelezi
Picha za skrini
Maelezo
Programu-jalizi ya kuwezesha otomatiki kwenye wavuti. Kiendelezi hiki cha wavuti kinaoana na Power Automate ya kompyuta, toleo la 2.27 au la baadaye.
Kiendelezi cha Microsoft Power Automate
Microsoft Power Automate hukuwezesha kuotomatisha michakato na kazi unazofanya mwenyewe kwenye kompyuta yako. Sakinisha kiendelezi hiki ili kuotomatisha shughuli kwenye wavuti kama vile kuendesha hati za programu, kuchimba data, kufanya majaribio, kujaza fomu na mengine mengi.
Zana ya kurekodi ya Power Automate itabadilisha hatua zako kuwa mtiririko wa kazi. Vinjari tu sehemu unazopenda za programu ya wavuti na ukusanye data, ujaze fomu, upakue faili – fanya mambo yote unayofanya kwa kawaida na uone mtiririko wa kazi ukiundwa.
Kiendelezi hiki cha kivinjari kinahitaji programu ya ziada ili kifanye kazi ipasavyo. Hakikisha kuwa umepakua na kusakinisha Power Automate kwenye kifaa chako kabla ya kuendelea.
Kumbuka: Baada ya tarehe maalumu ambayo itatangazwa rasmi na timu ya kivinjari, kivinjari hakitaauni tena viendelezi vya wavuti vilivyoundwa kwa Manifest V2. Kiendelezi hiki cha wavuti kimeanza kutumia Manifest V3 mpya na kinaoana na Power Automate, toleo la 2.27 au la baadaye. Ikiwa ungependa kusakinisha kiendelezi hiki cha wavuti, tafadhali hakikisha kuwa umeboresha Power Automate hadi toleo linalooana ili kuotomatisha shughuli za wavuti. Pata maelezo zaidi hapa: https://go.microsoft.com/fwlink/?linkid=2211532
Kwa kusakinisha kiendelezi hiki, unakubali Masharti yaliyo katika: https://docs.microsoft.com/dynamics365/legal/slt-power-automate-brsr