Toucan by Babbel - Language Learning
ID
lokjgaehpcnlmkebpmjiofccpklbmociJifunze lugha unapovinjari kwa kutafsiri maneno ya kurasa za wavuti, kuhifadhi msamiati na kufanya mazoezi mafupi.
Picha za skrini
Maelezo
Jifunze lugha mpya kwa kuvinjari intaneti tu.
Jifunze lugha mpya kwa njia ya asili
Toucan hukusaidia kujifunza lugha mpya kwa njia ya asili kwa kuziingiza katika shughuli zako za mtandaoni. Kwa sababu kadiri unavyoona na kusikia lugha mpya zaidi, ndivyo unavyojifunza kwa kasi zaidi.
Jinsi inavyofanya kazi
➤ Kila unapotembelea tovuti, Toucan hutafsiri baadhi ya maneno na vifungu vya maneno kuwa lugha unayojaribu kujifunza. Hivyo, unaweza kujifunza lugha yako mpya ukitumia vidokezo vya muktadha katika lugha unayoijua tayari.
Lugha zinazopatikana:
Kiingereza | Kihispania | Kifaransa | Kijapani | Kijerumani | Kikorea | Kireno | Kiitaliano | Kiarabu | Kichina (Mandarin) | Kiebrania | Kihindi
Vipengele vya Toucan
Kadiri unavyofanya mazoezi zaidi, ndivyo unavyojifunza kwa kasi zaidi. Kila mtu hujifunza kwa njia tofauti, kwa hiyo badala ya maswali ya kupima ujuzi, mitihani na alama, Toucan imeunda vipengele mbalimbali vya kukupa vipindi vidogo vya kujifunza kwa furaha siku nzima
➤ Shortcuts
Huhitaji kujua kila neno la lugha ili kuweza kuizungumza. Shortcuts ya Toucan hukufundisha maneno na vifungu vya maneno kwa hali za kawaida, kama kuagiza chakula kwenye mkahawa au kutafuta choo.
➤ Extra Practice
Extra Practice ya Toucan huingiza vipindi vifupi vya mazoezi katika Google, Twitter na Reddit. Kwa hiyo unaweza kumudu mnyambuliko wa vitenzi, sarufi na muundo wa sentensi ili lugha yako mpya ibaki akilini.
➤ Hifadhi maneno kwa ajili ya baadaye
Umeona tafsiri ambayo ungependa sana kukumbuka? Toucan hukusaidia kujifunza maneno yenye manufaa kwa kasi zaidi kwa kuyahifadhi ili uyapitie na kuyafanyia mazoezi baadaye.
Ukikumbana na tatizo lolote, unaweza kutuma barua pepe kwa [email protected] ili kupata msaada kutoka kwa timu yetu bora ya usaidizi kwa wateja.
*************** FARAGHA YAKO NDIYO KIPAUMBELE CHA KWANZA CHA TOUCAN ***************
Ingawa tuna uhakika kuwa wewe ni mtu wa kuvutia sana, Toucan haina nia ya kufuatilia tovuti unazotembelea, unachotafuta, unachonunua au kitu kingine chochote isipokuwa lugha unayojaribu kujifunza. Hiyo si kazi yetu.
Pata maelezo zaidi kuhusu sera ya faragha ya Toucan katika https://www.babbel.com/legal/privacy