Picha za skrini

Maelezo

Tazama maana za maneno kwa urahisi unapovinjari wavuti. MUHIMU: - Kiputo ibukizi hakitafanya kazi kwenye vichupo vilivyokuwa vimefunguliwa kabla ya usakinishaji. Baada ya kusakinisha kiendelezi hiki, pakia upya vichupo vyako vilivyo wazi au uanzishe upya Chrome. - Kumbuka kuwa viendelezi vyote vimezimwa kwenye kurasa za Chrome Web Store (ikiwemo hii). Usijaribu kiendelezi kwenye ukurasa huu; hakitafanya kazi! - Ikiwa kiendelezi hakifanyi kazi kwako, hakikisha kuwa kimesasishwa. Tembelea chrome://extensions/, bofya kitufe cha "Sasisha viendelezi sasa", kisha uanzishe upya Chrome. ---------- Kwa kiendelezi hiki, unaweza: 1) Kubofya mara mbili neno lolote ili kuona maana yake katika kiputo kidogo ibukizi. 2) Kuona maana kamili ya neno au kifungu chochote kwa kutumia kamusi iliyo kwenye upau wa vidhibiti. 3) Kuhifadhi historia ya maneno uliyotafuta, ili uweze kuyafanyia mazoezi baadaye. Maneno ya kigeni hutafsiriwa kiotomatiki katika lugha unayochagua. Kamusi zinazotumika: - Kiarabu - Kireno cha Brazili - Kichina (Kilichorahisishwa) - Kichina (cha Jadi) - Kicheki - Kiholanzi - Kiingereza (Uingereza) - Kiingereza (Marekani) - Kifaransa - Kijerumani - Kihindi - Kiitaliano - Kijapani - Kikorea - Kirusi - Kislovakia - Kihispania - Kituruki Ukiamua kuwasha kipengele hiki (kupitia ukurasa wa machaguo), kiendelezi hiki kitahifadhi historia ya maneno yote uliyotafuta pamoja na maana zake. Unaweza kupakua historia hii kama faili la CSV wakati wowote. Aidha, unaweza kuruhusu viendelezi vingine vya Chrome kufikia historia hii. Kwa mfano, kiendelezi kutoka kwa mhusika mwingine kinaweza kutengeneza kadi za kujifunzia ili kukusaidia kufanya mazoezi ya maneno uliyotafuta hapo awali. Kwa kusakinisha kiendelezi hiki, unakubali Sheria na Masharti ya Huduma: https://www.google.com/policies/terms Je, una matatizo na kiendelezi hiki? Ikiwa mapendekezo yaliyo hapo juu hayakusaidia, tafadhali jaza ripoti ya tatizo: https://chrome.google.com/webstore/support/mgijmajocgfcbeboacabfgobmjgjcoja