Picha za skrini

Maelezo

Ona tafsiri kwa urahisi unapovinjari wavuti. Kutoka kwa timu ya Google Translate. Angazia au bofya kulia kwenye sehemu ya maandishi, kisha ubofye aikoni ya kutafsiri iliyo kando yake ili kuyatafsiri kwa lugha yako. Pata maelezo zaidi kuhusu Google Translate kwenye https://support.google.com/translate. Kwa kusakinisha kiendelezi hiki, unakubali Sheria na Masharti ya Google pamoja na Sera ya Faragha zilizo kwenye https://www.google.com/intl/en/policies. SASISHO (v.2.0): Sasa unaweza kuangazia au kubofya kulia kwenye maandishi na kuyatafsiri badala ya kutafsiri ukurasa mzima. Unaweza pia kubadilisha mipangilio ya kiendelezi ili kuonyesha tafsiri kiotomatiki kila unapoangazia maandishi. SASISHO (v.2.14+): Utafsiri wa kurasa sasa umejengewa ndani ya vivinjari vya Chrome na hautumiki tena katika kiendelezi cha Google Translate. Tazama https://support.google.com/chrome/answer/173424 ili kujifunza jinsi ya kuutumia. SASISHO (v.2.1.18): - Kwa maandishi asilia au yaliyotafsiriwa ambayo hayatumii mfumo wa herufi za Kilatini, sasa tunaonyesha maandishi hayo kwa herufi za Kilatini - Usaidizi kamili wa Kikantoni, ikiwemo kitufe cha kusikiliza maandishi asilia