Picha za skrini

Maelezo

Kizuia maudhui chenye ufanisi. Huzuia matangazo, vifuatiliaji, programu za uchimbaji wa sarafu za kidijitali na mengineyo mara tu kinaposakinishwa. uBO Lite (uBOL) ni kizuia maudhui chenye ufanisi kinachotegemea MV3. Seti ya kanuni za chaguo-msingi inalingana na seti ya vichujio vya chaguo-msingi ya uBlock Origin: - Orodha za vichujio zilizojumuishwa ndani ya uBlock Origin - EasyList - EasyPrivacy - Peter Lowe’s Ad and tracking server list Unaweza kuwezesha seti zaidi za kanuni kwa kufungua ukurasa wa chaguo -- bofya aikoni ya _magurudumu ya gia_ kwenye paneli ibukizi. uBOL hutegemea kabisa kanuni zilizobainishwa. Hii inamaanisha kuwa uchujaji hauhitaji mchakato wa uBOL unaoendelea kufanya kazi daima, na uchujaji wa maudhui kwa kuingiza CSS/JS hufanywa kwa kutegemewa na kivinjari chenyewe badala ya kiendelezi. Hii inamaanisha kuwa uBOL yenyewe haitumii rasilimali za CPU/kumbukumbu wakati uzuiaji wa maudhui unaendelea -- mchakato wa service worker wa uBOL unahitajika _tu_ unapotumia paneli ibukizi au kurasa za chaguo.