Picha za skrini

Maelezo

Kidhibiti cha nywila kilicho salama na rahisi kutumia. Bila nywila kuu hutahitaji tena kukumbuka nywila. Yoti Password Manager hukusaidia: - Kufikia na kutumia taarifa zako za kuingia bila kulazimika kukumbuka nywila yoyote. - Kufikia na kutumia taarifa zako za kuingia kwa urahisi kwenye mifumo na vifaa mbalimbali kwa kutumia kidhibiti cha nywila. - Kujaza kiotomatiki taarifa zako za kuingia unapotembelea tovuti uzipendazo. - Kutengeneza nywila thabiti na za kipekee kwa kila akaunti yako ya mtandaoni kwa kutumia kidhibiti cha nywila. - Kufunga kiotomatiki taarifa zako za kuingia ili ziwe salama unapokuwa mbali na kompyuta yako. Unahitaji programu ya Yoti isiyolipishwa ili kutumia Yoti Password Manager. Hivyo ndivyo tunavyohakikisha kuwa wewe pekee ndiye unayeweza kufikia na kutumia nywila zako. Programu ya Yoti ni njia mpya ya kuthibitisha utambulisho wako, ikikupa utambulisho wa kidijitali unaoaminika wa kutumia mtandaoni na ana kwa ana. Unaweza kutumia programu ya Yoti kuunganisha kwa usalama kwenye Yoti Password Manager, kuifungua na kuifunga wakati wowote unapotaka. Zaidi ya watu milioni 2 tayari wamepakua programu ya Yoti, na maelfu zaidi wanaipakua kila siku. Tafuta tu “Yoti” katika maduka ya programu ya iOS au Android. Kulinda data yako ndilo kipaumbele chetu kikuu. Ili kulinda kila taarifa unayotupa unaposajili akaunti yako ya Yoti, iwe ni picha, tarehe ya kuzaliwa, anwani au nywila zako, tunaisimba kwa usimbaji wa AES 256-bit. Funguo za faragha zinazofungua data yako huhifadhiwa kwenye kifaa chako. Hakuna mwingine, hata Yoti, anayeweza kufikia funguo hizi.