Picha za skrini

Maelezo

Hulinda data yako. Utafutaji wa faragha wenye AI ya hiari, kuvinjari kwa faragha, na kuzuia matangazo. Katika DuckDuckGo, tunaamini kwamba njia bora ya kulinda taarifa zako binafsi dhidi ya wadukuzi, walaghai, na kampuni zinazoingilia faragha ni kuzuia taarifa hizo zisikusanywe kabisa. Ndiyo sababu mamilioni ya watu huchagua DuckDuckGo badala ya viendelezi vingine vya kivinjari ili kulinda utafutaji na kuvinjari kwao. Injini yetu ya utafutaji iliyojengewa ndani ni kama Google lakini haifuatilii utafutaji wako kamwe. Ulinzi wetu wa kuvinjari, kama vile kuzuia vifuatiliaji vya matangazo na vidakuzi, husaidia kuzuia kampuni nyingine zisikusanye data yako. Vipengele vyetu vya AI vilivyounganishwa na vya hiari, Search Assist na Duck.ai, hulinda faragha na havitumii data yako kamwe kufunza AI. Pia, kiendelezi chetu cha kivinjari ni cha bure — tunapata mapato kutokana na matangazo ya utafutaji yanayoheshimu faragha, si kwa kutumia data yako kujinufaisha. Rejesha udhibiti wa taarifa zako binafsi kwa kiendelezi cha kivinjari kilichoundwa kulinda data. VIPENGELE MUHIMU Linda Utafutaji Wako kwa Chaguomsingi: Sakinisha kiendelezi hiki nasi tutaweka DuckDuckGo Search kuwa injini yako ya utafutaji ya chaguomsingi na ukurasa wako wa mwanzo, ili uweze kutafuta mtandaoni kwa urahisi bila kufuatiliwa.  Linda Historia Yako ya Kuvinjari: Ulinzi wetu dhidi ya kupakiwa kwa vifuatiliaji vya wahusika wengine huzuia vifuatiliaji vingi kabla havijapakiwa, na kutoa ulinzi unaozidi kwa kiasi kikubwa ule unaotolewa na kivinjari kwa chaguomsingi.  Zungumza kwa Faragha na AI: Duck.ai hukuwezesha kufanya mazungumzo ya faragha na miundo ya AI ya wahusika wengine; sisi huondoa taarifa zinazoweza kukutambulisha katika mazungumzo hayo na hayatumiwi kamwe kufunza AI. Linda Barua Pepe Yako (Hiari): Tumia Email Protection kuzuia vifuatiliaji vingi vya barua pepe na kuficha anwani yako ya sasa ya barua pepe kwa kutumia anwani za @duck.com.   Lazimisha Usimbaji Fiche Kiotomatiki: Linda data yako dhidi ya watu wanaochunguza mawasiliano kwenye mitandao na Wi-Fi kwa kulazimisha tovuti nyingi kutumia muunganisho wa HTTPS.  Epuka Utambuzi kwa Alama za Kipekee: Fanya iwe vigumu zaidi kwa kampuni kuunda kitambulisho cha kipekee cha kukutambua kwa kuzuia majaribio ya kuunganisha taarifa kuhusu kivinjari na kifaa chako.  Zuia Vidakuzi vya Ufuatiliaji: huzuia vidakuzi vingi vya wahusika wengine visikufuatilie unapovinjari kutoka tovuti moja hadi nyingine. Ulinzi Dhidi ya Teknolojia ya Ufuatiliaji ya Chrome: Huzuia Google kutumia kivinjari chako kukusanya na kuuza data yako binafsi kwa mnada kupitia vifuatiliaji na teknolojia zao za hivi karibuni za kulenga matangazo (“Protected Audience API” na “Topics API”). Tunatoa aina nyingi za ulinzi ambazo hazipatikani katika vivinjari na viendelezi vingi, hata katika hali ya kuvinjari kwa faragha, zikiwemo ulinzi dhidi ya ufuatiliaji kupitia viungo, Global Privacy Control, na nyinginezo. Huhitaji kusubiri ili kudhibiti taarifa zako binafsi! Jiunge na mamilioni ya watu wanaotumia DuckDuckGo kulinda utafutaji, kuvinjari, na matumizi yao ya kila siku ya barua pepe. Soma zaidi kuhusu ulinzi wetu wa bure dhidi ya ufuatiliaji katika https://help.duckduckgo.com/privacy/web-tracking-protections Sera ya Faragha: https://duckduckgo.com/privacy/  Masharti ya Huduma: https://duckduckgo.com/terms Dokezo kuhusu Ulinzi Dhidi ya Vifuatiliaji vya Wahusika Wengine na Matangazo ya Utafutaji: ingawa kuna vikwazo fulani baada ya kubofya matangazo ya utafutaji, kutazama matangazo kwenye utafutaji wa DuckDuckGo hakutambulishi wewe ni nani. Pata maelezo zaidi hapa https://help.duckduckgo.com/privacy/web-tracking-protections ---------------------------------------------------------------- Ili kupata ulinzi bora zaidi wa faragha unaowezekana katika Chrome, tunapendekeza pia urekebishe mipangilio ya Chrome ambayo haiwezi kudhibitiwa na viendelezi. Ondoka kwenye akaunti katika Chrome na uzime kuingia kwenye akaunti katika Chrome https://support.google.com/chrome/answer/9159867?hl=en&ref_topic=7439538; Usisawazishe data ya historia yako na Chrome (nenda kwenye maelekezo ya “Ondoka kwenye akaunti na uzime usawazishaji”) https://support.google.com/chrome/answer/185277; Katika Vidhibiti vya Shughuli vya Google, zima “Shughuli za Wavuti na Programu” https://support.google.com/websearch/answer/54068?sjid=344786957015178031-NC Katika Mipangilio ya Matangazo ya Google, zima Matangazo yaliyobinafsishwa https://adssettings.google.com/ Unatafuta kivinjari chetu cha Mac au Windows? Unaweza kuvipakua hapa: https://duckduckgo.com/app Msimbo Huria: https://github.com/duckduckgo/duckduckgo-privacy-extension