Adblock Plus - free ad blocker
ID
cfhdojbkjhnklbpkdaibdccddilifddbZuia matangazo na vifuatiliaji vya wahusika wengine kwenye YouTube na tovuti nyingine, kwa mipangilio unayoweza kubinafsisha ya kuzuia na kuruhusu.
Maelezo ya kiendelezi
Picha za skrini
Maelezo
Ondoa matangazo kwenye YouTube na kila mahali pengine unapovinjari.
Adblock Plus ni miongoni mwa vizuia matangazo vya bure vinavyopendwa na kuaminiwa zaidi, ikiwa imepakuliwa zaidi ya mara milioni 500. Adblock Plus imekuwa kizuiamatangazo kinachopendwa na watumiaji tangu 2006, na hukuwezesha kuzuia matangazo na kufurahia hali bora ya kuvinjari kwenye YouTube na tovuti zako nyingine uzipendazo.
Unatafuta kizuiamatangazo mbadala cha uBlock Origin? Tunaendana na Chrome kwa masasisho ya hivi karibuni ya MV3, na tutaendelea kuendana nayo daima.
➤ Pakua Adblock Plus na upate vipengele hivi vya bure vya kuzuia matangazo:
● Zuia matangazo yanayokera kama vile madirisha ibukizi, matangazo ya video na mabango ya matangazo.
● Zuia vifuatiliaji vya wahusika wengine na ulinde zaidi faragha ya taarifa zako dhidi ya watangazaji.
● Punguza ulaghai wa mtandaoni unaotokana na matangazo hasidi yenye virusi na ulaghai wa kuhadaa ili kuiba taarifa, ambao huhatarisha kifaa chako na kulenga akaunti zako.
● Binafsisha kuvinjari kwako kwa kuchagua unachotaka kuzuia na unachotaka kuruhusu.
● Furahia msaada wa bure na wa haraka kutoka kwa timu yetu!
➤ Pata manufaa zaidi kutoka kwa kizuiamatangazo chako na udhibiti zaidi wa kuvinjari kwako unapoboresha hadi Premium:
● Zuia zaidi ya matangazo na uachane na video zinazocheza kiotomatiki na kukufuata unapovinjari, madirisha ibukizi ya kujiandikisha kwa majarida ya habari, maombi ya kushiriki tafiti na mengineyo.
● Ficha mabango ya vidakuzi na ufike unakokwenda haraka zaidi unapokoma kuona madirisha yale ibukizi yanayokera yanayokuomba ukubali vidakuzi kwenye tovuti.
Adblock Plus hufanya kazi kama kizuiamatangazo cha YouTube na tovuti nyingine mara tu unaposakinisha kiendelezi, na kukuwezesha kuvinjari wavuti utakavyo. Unaweza kubinafsisha mipangilio yako baada ya kusakinisha kiendelezi, kukibandika kwenye upau wako wa zana na kufungua menyu. Katika hali fulani, matangazo yanaweza kuonyeshwa kwenye YouTube au tovuti nyingine. Pata maelezo zaidi kuhusu kuzuia matangazo kwenye YouTube: https://adblockplus.org/youtube. Ikiwa unahitaji kusitisha AdBlock Plus kwa muda, fungua kiendelezi na ubofye ‘sitisha kwenye tovuti hii’.
Kiendelezi chetu husaidia kuhakikisha maudhui yanaendelea kupatikana bila malipo kwa watumiaji kwa kuonyesha, kwa chaguomsingi, baadhi ya matangazo yasiyosumbua yanayokidhi Acceptable Ads Standard (www.acceptableads.com). Ikiwa hutaki kuona Acceptable Ads, unaweza kuzima chaguo hili wakati wowote: https://adblockplus.org/acceptable-ads#optout.
Tafadhali kumbuka: Unaposakinisha Adblock Plus, utapokea onyo kwamba kiendelezi kitaweza kufikia historia na data zako za kuvinjari. Huu ni ujumbe wa kawaida — KAMWE hatukusanyi taarifa zozote zinazoweza kumtambulisha mtumiaji.
Tunatanguliza faragha na usalama wa watumiaji, tukihakikisha historia yako ya kuvinjari na taarifa zako binafsi zinabaki kuwa za faragha. Kwa kupakua na kusakinisha kiendelezi hiki, unakubali Masharti yetu ya Matumizi: https://adblockplus.org/terms na Sera yetu ya Faragha https://adblockplus.org/privacy.
Kiendelezi hiki cha kuzuia matangazo kinapatikana pia kwa Firefox, Microsoft Edge na Opera.