Polarr Photo Editor
ID
djonnbgfieijldcieafgjcnhmpcfpmggHariri picha bila intaneti kwenye ChromeOS ukitumia vichujio, tabaka, barakoa, marekebisho ya maeneo maalumu na kuhamisha picha nyingi kwa pamoja.
Maelezo ya kiendelezi
Picha za skrini
Maelezo
Zana yenye nguvu zaidi ya kuhariri picha kwenye Chrome. Inafanya kazi bila intaneti.
Barua pepe yetu ya usaidizi ni [email protected]. Programu ilisasishwa mara ya mwisho tarehe 18 Novemba 2019.
Polarr ndiyo kihariri pekee cha picha unachohitaji.
Iwe wewe ni mgeni katika upigaji picha au mtaalamu, Polarr ina kila kitu. Wanaoanza watafurahia zana za hali ya juu za kuboresha picha kiotomatiki na vichujio bora vya Polarr vya kuhariri kila undani wa picha. Wapigapicha wataalamu wanaweza kutazamia matumizi ya tabaka, zana za mikunjo, marekebisho ya maeneo maalumu na mengi zaidi.
Ni kihariri chenye nguvu cha picha kwa ChromeOS. Hivi ndivyo unavyopata ukiwa na Polarr:
Muhtasari
• Tabaka za juu unazobinafsisha na hali changamani za kuchanganya
• Athari za lenzi mbili na marekebisho ya kina
• Seti kamili ya zana za barakoa na marekebisho ya maeneo maalumu
• Unda, binafsisha na shiriki vichujio vyako mwenyewe
• Kuhamisha picha nyingi kwa pamoja
Vichujio
• Tengeneza na shiriki vichujio vyako vilivyobinafsishwa
• Anza kwa vichujio vya msingi, kisha endelea kwa vya kitaalamu
• Sawazisha vichujio kwenye vifaa vyako vyote
Tabaka na hali za kuchanganya
• Weka picha juu ya nyingine kwa hali 10 au zaidi za kuchanganya
• Ongeza athari zinazoonekana halisi kama mawingu, athari za hali ya hewa, kuvuja kwa mwanga, miale ya lenzi na nyinginezo
• Tumia toni mbili kwenye picha kwa mipangilio yetu iliyowekwa tayari au unda mtindo wako wa kipekee
Marekebisho ya maeneo maalumu yanajumuisha
• Barakoa ya kina: rekebisha picha kulingana na kina kwa kutumia kamera mbili
• Barakoa ya brashi: chora barakoa yako
• Barakoa ya rangi: marekebisho teule kwa kutumia rangi
• Barakoa ya duara: marekebisho ya mviringo kwenye picha yako
• Barakoa ya mpito: kurekebisha picha kwa mpito wa taratibu
• Barakoa ya mwangaza: marekebisho teule kulingana na mwangaza.
• Zana nyingine za maeneo maalumu: ukungu wa lenzi, kulainisha kingo, kugeuza uteuzi na zaidi
• Changanya barakoa yoyote ya marekebisho ya eneo maalumu na tabaka la juu
• Weka marekebisho ya maeneo maalumu juu ya mengine bila kikomo.
Marekebisho ya picha nzima yanajumuisha
• Uboreshaji mahiri wa kiotomatiki wa mfiduo na usawazishaji wa weupe
• Rangi: halijoto, mwelekeo wa rangi, uchangamfu, ukolezi
• Mwanga: kuondoa ukungu, mfiduo, mwangaza, utofautishaji, sehemu zenye mwanga mwingi, vivuli, toni nyeupe, toni nyeusi, usambazaji wa mwanga
• Undani: uwazi, kunoa picha, kupunguza kelele za picha (rangi na mwangaza)
• Kufifisha pembe: kiasi, sehemu zenye mwanga mwingi, umviringo
• Lenzi: upotoshaji, mtazamo wa mlalo na wima
• Athari: mipaka yenye rangi, kugawa picha katika pikseli kubwa, kiasi na ukubwa wa kelele za picha
• HSL: aina ya rangi, ukolezi na mwangaza kwa chaneli nane za rangi
• Mikunjo: chaneli kuu, ya buluu, nyekundu na kijani
• Toni: toni za sehemu zenye mwanga mwingi na vivuli, kusawazisha toni
• Kupunguza kelele za picha: ulengaji, uboreshaji na uwazi
• LUT: ingiza na hamisha 3D Lut (iOS 11 au matoleo mapya zaidi)
Polarr inaweza kubinafsishwa
• Chagua mandhari meusi, angavu au ya rangi ulizobinafsisha
• Maeneo mawili ya kazi yanapatikana: Pro na Express
• Panga upya aikoni ili programu ikufae
Inafanya kazi kwenye vifaa vyako vyote
• Polarr inapatikana kwa vifaa vyako vyote: simu, kompyuta na wavuti
• Usajili wako wa pro unakufuata kwenye vifaa vyako vyote
Tembelea tovuti yetu https://www.polarr.co ili kuona bidhaa zetu zote bora.
Tuma barua pepe kwa [email protected] kwa maswali yoyote.