Picha za skrini

Maelezo

Fanya mengi zaidi katika Google Chrome ukitumia zana za PDF za Adobe Acrobat. Tazama, jaza, toa maoni, tia sahihi, na ujaribu zana za kubadilisha miundo na kubana faili. Adobe Acrobat ni suluhisho linaloongoza katika tasnia ya PDF, linalotumiwa na mamilioni ya watu. Tumia zana za PDF za Acrobat moja kwa moja katika Google Chrome ili upate hali bora zaidi ya kutazama PDF na ufanye mengi zaidi unapovinjari. Unaweza kuongeza maoni kwenye PDF, yakiwemo madokezo yanayobandikwa, maandishi na uangaziaji wa maandishi—yote bila malipo. Ikiwa unahitaji vipengele vya juu zaidi vya Acrobat, unaweza kujaribu zana za kubadilisha PDF kuwa miundo mingine na miundo mingine kuwa PDF, kuunda PDF, kuunganisha hati za PDF, kupanga PDF, kupunguza ukubwa wa PDF, na zaidi. Kufanya kazi na PDF mtandaoni hakujawahi kuwa rahisi hivi. JINSI YA KUTUMIA KIENDELEZI CHA ACROBAT CHA CHROME 1. Sakinisha kiendelezi cha Acrobat cha Chrome. 2. Bandika kiendelezi ili ukifikie haraka. 3. Fungua PDF yoyote katika kivinjari chako. 4. Chagua zana ya Acrobat. TAZAMA, PAKUA, CHAPISHA NA HIFADHI PDF • Pata hali bora zaidi ya kutazama PDF ukitumia kisomaji cha PDF cha Acrobat. • Pakua au chapisha kwa mbofyo mmoja wa haraka. • Ingia katika akaunti ili uhifadhi faili zako mtandaoni na ufikie faili za PDF haraka kutoka popote. HARIRI PDF KWA KUONGEZA MAONI BILA MALIPO • Ongeza madokezo, maandishi na maoni kwenye PDF, yakiwemo madokezo yanayobandikwa na uangaziaji wa maandishi. • Andika kwenye hati za PDF kwa kuongeza maandishi au michoro ukitumia vipengele vya kihariri cha PDF. JAZA NA UTIE SAHIHI FOMU BILA MALIPO • Fungua PDF katika Adobe Acrobat Reader ili ujaze na kutia sahihi fomu kwenye kompyuta yako. • Jaza fomu za PDF kwa urahisi ukitumia kipengele cha Acrobat cha kujaza fomu. • Tia sahihi hati kielektroniki kwa kutumia sahihi yako au herufi za mwanzo za majina yako. JARIBU ZANA ILI UFANYE KAZI KWA UFANISI ZAIDI KATIKA CHROME Jaribu zana za kulipia ili upate uwezo zaidi wa kufanya kazi na PDF. • Tumia zana yetu ya kubadilisha miundo ya PDF ili ubadilishe PDF kuwa miundo ya Microsoft Word, Excel na PowerPoint na miundo hiyo kuwa PDF, pamoja na JPG na miundo mingine ya faili kuwa PDF na kinyume chake. • Unda PDF kutoka kwenye hati au picha, ikiwa ni pamoja na kubadilisha JPG kuwa PDF. • Unganisha faili kuwa faili moja ya PDF au ugawanye PDF. • Panga PDF yako. Futa, zungusha au badilisha mpangilio wa kurasa za PDF. • Bana PDF ili kupunguza ukubwa wa faili yake. • Tuma hati kwa wengine ili wazitie sahihi kielektroniki mtandaoni kwa haraka. • Linda hati ya PDF kwa kuongeza nenosiri. Unaweza pia kujisajili kwa kipindi cha majaribio bila malipo kwenye https://www.adobe.com/tryacrobat. MAPYA: • Hariri PDF zako katika kitazamaji cha Acrobat cha Chrome • Jaza na utie sahihi fomu bila malipo • Uwezo wa kufungua faili za PDF zilizohifadhiwa kwenye kifaa katika kiendelezi Sheria na Masharti: Matumizi yako ya programu hii yanatawaliwa na Masharti ya Jumla ya Matumizi ya Adobe (http://www.adobe.com/go/terms_en) na Sera ya Faragha ya Adobe (http://www.adobe.com/go/privacy_policy_en), pamoja na matoleo yoyote yatakayochukua nafasi yake.