Picha za skrini

Maelezo

Hifadhi maudhui ya wavuti au picha ya skrini moja kwa moja kwenye Google Drive. Kiendelezi cha Chrome cha Save to Google Drive hukusaidia kuhifadhi maudhui ya wavuti au picha za skrini ya kivinjari kwenye Google Drive yako. * Huongeza kitufe cha kivinjari cha kuhifadhi ukurasa wa sasa. * Huongeza menyu ya kubofya kulia ili kuhifadhi viungo na maudhui ya media. * Kinaweza kusanidiwa kupitia ukurasa wa chaguo. * Hifadhi ukurasa wa sasa kama PDF kupitia menyu ya Kuchapisha ya Chrome Kiendelezi hiki hukuwezesha kuhifadhi maudhui ya wavuti moja kwa moja kwenye Google Drive kupitia kitufe cha kivinjari au menyu ya muktadha. Unaweza kuhifadhi hati, picha, pamoja na sauti na video za HTML5 kwa kubofya kulia na kuchagua 'Save to Google Drive'. Unaweza kuhifadhi ukurasa unaoutazama kwa kutumia kitufe cha kivinjari cha 'Save to Google Drive' au kama PDF kupitia menyu ya Kuchapisha ya Chrome.. Mahali pa folda na muundo wa kurasa za HTML zilizohifadhiwa vinaweza kuwekwa kupitia ukurasa wa chaguo wa kiendelezi (chaguo ni picha ya ukurasa mzima (chaguo-msingi), picha ya sehemu inayoonekana, HTML ghafi, MHTML, au hati ya Google). Unaweza kubadilisha kiotomatiki faili za Microsoft Office au faili zenye thamani zilizotenganishwa kwa koma kuwa muundo wa Google Docs. Baada ya maudhui yako kuhifadhiwa, kisanduku cha mazungumzo cha maendeleo hukuwezesha kufungua faili, kuipa jina jipya, au kuiona katika orodha ya hati ya Google Drive. Kutoka kwenye orodha ya hati, unaweza kupanga na kushiriki hati yako mpya. Ili kuhifadhi anwani za file://, au kuwezesha kiendelezi katika hali fiche, nenda kwenye chrome://extensions/ na uweke alama kwenye kisanduku cha kuteua kinachohusika. Kutokana na vizuizi vya usalama, kiendelezi hiki hakiwezi kupiga picha za kurasa za chrome:// au kurasa za Chrome Web Store. Mapya katika Toleo la 2.3.8: * Hurekebisha hitilafu ya uidhinishaji. Mapya katika Toleo la 2.3.2: * Hurekebisha hitilafu iliyosababisha baadhi ya faili za PDF kuhifadhiwa bila kiendelezi cha jina la faili. Mapya katika Toleo la 2.3.1: * Marekebisho ya hitilafu. * Huwezesha kuchapisha ukurasa wa sasa kutoka Google Chrome kwenda Google Drive kama PDF. Kumbuka: Kwa sasa Google Chrome hutoa kipengele hiki ndani yake, lakini hivi karibuni kipengele hicho kilichojengewa ndani kitabadilishwa kabisa na kipengele sawa cha Kiendelezi hiki cha Chrome. Mapya katika Toleo la 2.1.1: Marekebisho ya hitilafu. Mapya katika Toleo la 2.1: Uidhinishaji sasa unahitaji uwe umeingia katika Chrome. Ili kuhifadhi kwenye akaunti tofauti ya Google Drive, lazima ubadilishe wasifu wa Chrome. Mapya katika Toleo la 2.0.1: Marekebisho ya hitilafu iliyosababisha ukurasa wa uthibitishaji kuelekezwa kwenye about:blank baada ya kubofya Kubali. Mapya katika Toleo la 2: * Hutumia mchakato wa uthibitishaji wa OAuth2, kwa hivyo utahitaji kuthibitisha utambulisho wako tena unapokitumia kwa mara ya kwanza * Uwezo wa kuchagua folda lengwa (huwekwa kwenye ukurasa wa Chaguo) * Usaidizi kwa thamani kubwa za devicePixelRatio (skrini za Chrome Pixel na Retina) * Kubofya jina la folda ambamo faili imehifadhiwa huonyesha faili iliyopakiwa hivi punde katika folda lengwa * Chaguo huhifadhiwa katika hifadhi ya pamoja, kwa hivyo husawazishwa kati ya vivinjari ikiwa Chrome Sync imewezeshwa. Kwa kusakinisha kipengee hiki, unakubali Sheria na Masharti ya Google na Sera ya Faragha iliyo kwenye https://www.google.com/intl/en/policies/.