Co:Writer
ID
ifajfiofeifbbhbionejdliodenmecnaPata msaada wa kuandika mtandaoni kwa utabiri wa maneno unaozingatia sarufi, msaada wa tahajia, utambuzi wa sauti na usomaji wa maandishi kwa sauti.
Maelezo ya kiendelezi
Picha za skrini
Maelezo
Utabiri wa maneno unaozingatia sarufi na kutambua tahajia za kubuni. Utambuzi wa sauti hukuwezesha kusema unachotaka kuandika, nasi tutakiandika.
Kiendelezi cha Co:Writer® Universal kwa Chrome™ hukusaidia kuandika kwa sarufi na tahajia sahihi ukitumia msamiati unaohusu mada maalumu. Kinaunganishwa na kivinjari cha Chrome™ ili kutoa utabiri wa maneno na utambuzi wa sauti karibu popote unapoandika mtandaoni, ikiwa ni pamoja na Google Drive™, Microsoft Word, blogu, mifumo ya usimamizi wa ujifunzaji, mitihani, mitandao ya kijamii na barua pepe.
Kijaribu bila malipo uone kama kinakufaa. Bei na maelezo zaidi yanapatikana kwenye https://cowriter.com
Co:Writer Hufanyaje Kazi?
Unapoandika herufi, Co:Writer hutabiri neno unalokusudia na kuonyesha mapendekezo kadhaa ya maneno kwa kutumia utabiri madhubuti unaozingatia sarufi. Mapendekezo haya yanaweza kusomwa kwa sauti kwa kusogeza kishale juu ya maneno. Kuchagua neno unalokusudia huliingiza katika hati ya kuandikia iliyojengewa ndani. Ili kusikiliza ulichoandika unapoandika (na baada ya kuandika), unaweza kutumia kipengele kilichojengewa ndani cha kusoma maandishi kwa sauti ili kusoma herufi, maneno, sentensi na maandishi yoyote yaliyochaguliwa. Ukichagua maikrofoni, unaweza kuzungumza nasi tutabadilisha usemi wako kuwa maandishi.
Zaidi ya Kamusi Milioni 4 za Mada Maalumu:
Co:Writer inaweza kufikia kamusi kuu ya utabiri wa maneno (inayojumuisha maneno ya msingi) na Kamusi za Mada (zinazojumuisha maneno yanayohusu mada maalumu). Co:Writer inaweza kufikia zaidi ya kamusi milioni 4 za mada maalumu, ambazo huwashwa kulingana na kazi ya kuandika.
Mifano michache ya aina mbalimbali za kamusi za mada:
✔ America's Cup
✔ Kulinganisha na Kutofautisha
✔ Dinosauri
✔ Grumpy Cat
✔ Historia ya Vita vya Peloponnesi
✔ Mahatma Gandhi
✔ Mbwa Wangu
✔ Pig Latin
✔ SpongeBob SquarePants
✔ Tommy (albamu)
✔ Maajabu ya Dunia
Msaada wa Tahajia:
Co:Writer hutumia teknolojia ya Flexspell™ kushughulikia aina nyingi zaidi za makosa ya tahajia kuliko zote, yakiwemo kuandika maneno kulingana na yanavyosikika na makosa ya tahajia za kubuni (kuacha herufi, kuacha viishio vya maneno, kubadilisha mpangilio wa herufi, n.k.).
Mifano ya jinsi Co:Writer inavyosaidia kwa tahajia zinazofuata sauti na/au tahajia za kubuni:
Kabla ya Co:Writer:
The blk jargon flu over the bra lfnt.
R u hpy to ce me?
I no hw to nor the fone.
Baada ya Co:Writer:
The black dragon flew over the gray elephant.
Are you happy to see me?
I know how to answer the phone.
Msaada wa Sarufi:
Co:Writer hutegemea sarufi sahihi kutabiri maneno, na hutumia uelewa wake wa sarufi kutabiri maneno kwa usahihi ndani ya miundo sahihi ya sentensi.
Mifano ya jinsi Co:Writer inavyosaidia kwa sarufi:
Dogs are furry. (nomino, kitenzi, kivumishi) - Unapoandika d-o, unapewa chaguo za nomino za wingi
Three very mangy dogs ran down the street. (kivumishi, kielezi, kivumishi, nomino, kitenzi… n.k.) - Baada ya kuandika three, very, mangy, unapewa chaguo za nomino za wingi, kisha unapewa miundo ya vitenzi katika nyakati mbalimbali kwa wingi.