Picha za skrini

Maelezo

Ongeza kujiamini katika kusoma na kuandika kwenye aina zote za maudhui na vifaa, darasani, kazini na nyumbani. Read&Write for Google Chrome™ ni rahisi sana kuelewa na kutumia, na hutoa usaidizi unaokufaa binafsi ili kufanya hati, kurasa za wavuti na aina za faili zinazotumiwa sana kwenye Google Drive (zikiwemo: Google Docs, PDF na ePub) ziwe rahisi zaidi kufikia na kutumia. Imeundwa kumsaidia kila mtu kutumia maudhui ya kidijitali kwa njia inayolingana na uwezo wake na mitindo yake ya kujifunza. Read&Write hutoa zana mbalimbali zenye uwezo mkubwa za kukusaidia kujiamini katika kusoma, kuandika, kujifunza na kufanya utafiti, zikiwemo: • Usomaji wa maandishi kwa sauti ili kusikiliza maneno, vifungu au hati nzima zikisomwa kwa sauti, huku maandishi yakiangaziwa kwa rangi mbili zinazorahisisha kufuatilia • Kamusi za maandishi na picha ili kuona maana za maneno zikifafanuliwa • Kwa kutumia ubadilishaji wa sauti kuwa maandishi, tamka maneno ili yaandikwe na kukusaidia kuandika, kusahihisha maandishi na kujifunza • Utabiri wa maneno hutoa mapendekezo ya neno la sasa au linalofuata unapoandika • Kusanya sehemu za maandishi ulizoangazia kwenye hati au wavuti kwa ajili ya kutengeneza muhtasari na kufanya utafiti • Unda na usikilize madokezo ya sauti moja kwa moja ndani ya Google Docs • Rahisisha na ufupishe maandishi kwenye kurasa za wavuti ili kuondoa matangazo na maandishi mengine yanayoweza kuvuruga umakini Sakinisha Read&Write for Google Chrome ili utumie vipengele hivi VYOTE BILA MALIPO kwa siku 30! Walimu wanaweza kupata usajili wa premium wa Read&Write for Google Chrome BILA MALIPO. Ili kujisajili na kuamilisha usajili wako, nenda kwenye texthelp.com/en-gb/products/read-write/free-for-teachers/ baada ya kusakinisha toleo la majaribio la Read&Write for Google Chrome. Pata maelezo zaidi kuhusu vipengele, leseni na bei za Read&Write for Google Chrome™ kwenye texthelp.com/en-gb/products/read-write/premium-features/