Picha za skrini

Maelezo

Kiendelezi cha Chrome cha Ununuzi hurahisisha mchakato wa kuwekea bidhaa lebo kwenye YouTube. Hifadhi bidhaa, angalia viwango vya mgawo wa asilimia ya mauzo na uone mapendekezo mbadala unapovinjari tovuti yoyote ya biashara ya mtandaoni. Mpango wa washirika wa Ununuzi kwenye YouTube hukusaidia kubuni hali ya ununuzi isiyo na usumbufu kwa mashabiki wako na kuchuma mapato zaidi watazamaji wanaponunua bidhaa ulizowekea lebo kwenye video zako. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kujisajili na iwapo unatimiza masharti katika Kituo cha Usaidizi. Ukitumia kiendelezi cha Ununuzi kwenye YouTube, unaweza kurahisisha zaidi mchakato wa kuweka lebo. Vinjari tu chapa na wauzaji wa rejareja unaowapenda na tutakuletea maelezo na zana unazohitaji: - Hifadhi bidhaa: Hifadhi bidhaa unapovinjari tovuti ya chapa au muuzaji wa rejareja sasa, ili uweze kuzipata kwa urahisi utakapokuwa tayari kuziwekea lebo kwenye video yako katika Studio baadaye. - Angalia mgawo wa asilimia ya mauzo: Gundua ni kiasi gani utapata kutokana na kuwekea lebo bidhaa hiyo kwenye video zako za YouTube bila kuondoka kwenye tovuti ya chapa au muuzaji wa rejareja. - Ongeza mapato: Unaweza pia kuangalia bidhaa zinazofanana zinazotoa viwango vya juu vya mgawo wa asilimia ya mauzo kutoka kwa wauzaji wengine.