Picha za skrini

Maelezo

Tafuta makala za kitaaluma unapovinjari wavuti. Kiendelezi hiki huongeza kitufe kwenye kivinjari ili ufikie Google Scholar kwa urahisi kutoka ukurasa wowote wa wavuti. Bofya kitufe cha Scholar ili: - Kupata matini kamili kwenye wavuti au katika maktaba ya chuo kikuu chako. Chagua kichwa cha makala kwenye ukurasa unaousoma, kisha ubofye kitufe cha Scholar ili kuipata. - Kuhamisha hoja yako ya utafutaji kutoka utafutaji wa wavuti hadi Scholar. Bonyeza kitufe cha Scholar ili kuona matokeo matatu ya kwanza; bofya "skrini nzima" chini ya dirisha ibukizi ili kuyaona yote. - Kupangilia marejeleo kwa mitindo ya kunukuu inayotumiwa sana. Bonyeza kitufe cha alama za kunukuu kilicho chini ya tokeo ili kuona rejeleo lililopangiliwa na kulinakili kwenye makala unayoandika. - Kuhifadhi makala kwenye maktaba yako ya Scholar, ili uweze kuisoma au kuirejelea baadaye. Bonyeza nyota ya bluu chini ya tokeo ili kuihifadhi, au nyota ya kijivu iliyo chini ili kuona makala zote zilizohifadhiwa. Viungo vya maktaba hufanya kazi vizuri zaidi ukiwa chuoni. Ili kuvisanidi kwa matumizi nje ya chuo, tembelea Mipangilio ya Google Scholar kwenye https://scholar.google.com/scholar_settings (huenda ukahitaji kuingia kwa kutumia nenosiri la maktaba yako au kusanidi kivinjari chako kitumie proksi ya maktaba; tafadhali tembelea tovuti ya maktaba yako au uombe msaada kwa mhudumu wa maktaba aliye karibu nawe). Ili kutafuta sheria zinazotokana na maamuzi ya mahakama za Marekani, bofya aikoni ya gia iliyo chini ya dirisha ibukizi, kisha usanidi mkusanyiko unaopendelea katika Mipangilio ya Google Scholar. Kwa kusakinisha kiendelezi hiki, unakubaliana na Sheria na Masharti ya Google pamoja na Sera yake ya Faragha kwenye https://www.google.com/intl/en/policies/.