Picha za skrini

Maelezo

Tafuta kuponi na ofa kutoka kwa maduka na tovuti zinazoaminika. Zitatumika kiotomatiki kwa niaba yako unapolipia. Ununuzi wa busara sasa umekuwa wa busara zaidi ukiwa na kiendelezi cha AVG SafePrice. Hizi ndizo sababu zinazokifanya kuwa kifaa chako muhimu cha kutafuta bei bora: 💰 Akiba isiyo na kifani - AVG SafePrice hutafuta kwenye intaneti ili kukusaidia kupata kuponi katika maduka yako ya mtandaoni unayoyapenda. 🔐 Tovuti zinazoaminika pekee - Kuwa na amani ukijua kwamba tunakagua tovuti zinazoaminika pekee, ili uweze kununua kwa kujiamini bila kuhofia ulaghai au udanganyifu. Ukiwa na AVG SafePrice, daima uko mikononi salama. ✅Kuangazia ofa bora - Kiendelezi chetu huangazia ofa za bei nafuu zaidi ambazo zitakuokoa pesa nyingi zaidi, ili ununue kwa busara na kuongeza akiba yako kadiri iwezekanavyo. 💡Upau wa zana usiokusumbua - Upau wetu wa zana hubaki umefichwa usipokuwa unanunua, hivyo kupunguza visumbufu na kuweka hali yako ya kuvinjari bila msongamano wa vitu visivyohitajika. Sasa ni wakati wa kujaribu ununuzi wa busara zaidi kwa AVG SafePrice. Pakua sasa na uanze kuokoa pesa kwenye ununuzi mtandaoni! Ukiwa na swali au tatizo lolote, tafadhali tembelea: https://support.avg.com/ Taarifa kuhusu ushirika wa mauzo: AVG SafePrice hushiriki katika programu za ushirika wa mauzo. Hii inamaanisha kwamba tunaweza kupata kamisheni unapobofya viungo katika kiendelezi chetu, bila gharama yoyote ya ziada kwako. Kamisheni hizi husaidia kuendeleza bidhaa yetu. Masharti Kwa kusakinisha kiendelezi hiki kwenye kivinjari chako, unathibitisha kuwa umesoma na kukubali Sera ya Faragha ya AVG (https://avg.com/privacy) na Mkataba wa Leseni ya Mtumiaji wa Mwisho (https://www.avg.com/en-us/eula), ambazo husimamia upakuaji na matumizi yako ya bidhaa uliyochagua.