Picha za skrini

Maelezo

Ingia katika tovuti zinazotumika kwa akaunti zako za Microsoft za kazini au shuleni kwenye Windows na macOS. Tumia kiendelezi hiki kuingia katika tovuti zinazotumika kwa akaunti za Microsoft za kazini au shuleni kwenye Windows (10 na matoleo ya baadaye) au macOS (11 na matoleo ya baadaye). Ikiwa una Microsoft Entra ID kwenye kompyuta yako ya Windows au macOS, kiendelezi hiki huboresha uwezo wa kuingia mara moja ili kufikia tovuti zinazotumika. Bado unaweza kuona maombi ya ziada ya kuthibitisha utambulisho, kama vile uthibitishaji kwa njia nyingi, kutegemea mahitaji ya ufikiaji ya programu, rasilimali na mashirika mbalimbali. Kiendelezi hiki kinahitajika kwa sera fulani za ufikiaji wenye masharti unaotegemea kifaa kwa Microsoft Entra ID. https://learn.microsoft.com/en-us/entra/identity/conditional-access/concept-conditional-access-conditions#supported-browsers Kwa macOS, kiendelezi hiki kinahitaji kifaa kiwe kinasimamiwa, na pia Company Portal isakinishwe kando: https://learn.microsoft.com/en-us/mem/intune/user-help/enroll-your-device-in-intune-macos-cp Kumbuka: Ikiwa unapata matatizo ya kuingia au kufikia rasilimali, huenda yanahusiana na sera za vifaa za shirika lako. Tafadhali wasilisha tiketi ya usaidizi moja kwa moja kwa Microsoft kupitia usajili wa mazingira ya shirika lako (tenant). Anwani ya barua pepe ya msanidi programu wa kiendelezi si njia ya kupata usaidizi kwa wateja.