Phantom
ID
bfnaelmomeimhlpmgjnjophhpkkoljpaDhibiti sarafu za kidijitali na NFT kwenye Solana, Ethereum na Polygon, ukiwa na ubadilishaji wa tokeni, staking na historia ya miamala.
Maelezo ya kiendelezi
Picha za skrini
Maelezo
Pochi ya sarafu za kidijitali iliyobuniwa upya kwa DeFi na NFT
Phantom ni mwandamani wako unayemwamini kwa web3.
Pochi yetu inayotumia minyororo mingi ya bloku hukusaidia kuchunguza web3, kutumia programu, na kununua, kuhifadhi na kufanya biashara ya sarafu za kidijitali na NFT kwenye Solana, Ethereum na Polygon.
Ni rahisi, salama na ya kufurahisha. Kwa kila mtu.
Huweka kila kitu mahali pamoja
- Tumia minyororo mingi ya bloku kwa pochi moja. Hakuna haja ya kubadilisha mitandao mwenyewe.
- Fikia masoko makubwa zaidi ya NFT bila usumbufu.
- Tazama na onyesha mkusanyiko wako wa NFT.
- Fuatilia shughuli zote kwa historia ya kina ya miamala na arifa.
- Hakuna vikomo vya tokeni, salio au miamala.
Zana zenye uwezo mkubwa zilizoundwa kwa kila mtu
- Fanya mengi zaidi kwa NFT zako – zibandike, zifiche, ziteketeze na ziorodheshe kwa mauzo, yote ukiwa ndani ya pochi yako.
- Badilisha tokeni kwa kasi kubwa na kwa ada ndogo.
- Hifadhi tokeni zako, ziweke kwenye staking na upate zawadi.
- Orodhesha NFT zako kwa mauzo kwa urahisi kwenye masoko ya NFT moja kwa moja kutoka Phantom.
- Nunua sarafu za kidijitali kutoka vyanzo zaidi ya 7, vikiwemo malipo kwa kadi na uhamisho wa benki.
Usalama wa kiwango cha juu katika aina yake
- Kwa kuwa hii ni pochi ambayo unahifadhi mali zako mwenyewe, una udhibiti kamili wa fedha zako. Sisi hatuwezi kamwe kuzifikia.
- Imeundwa kulinda faragha. Huhitaji kutoa jina, barua pepe au namba ya simu.
- Mfumo wa kugundua ulaghai huashiria miamala yenye nia mbaya mara moja.
- Unganisha Ledger yako kwa usalama zaidi.
- Timu yetu ya usaidizi ya kimataifa iko hapa kwa ajili yako saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki.
Pakua Phantom ili uanze kuchunguza web3 leo.