Picha za skrini

Maelezo

Kichujio bora cha maombi ya mtandao kinachotumia kumbukumbu na CPU kwa kiwango kidogo sana. Kichujio bora cha maombi: kinatumia kumbukumbu na CPU kidogo sana na, kikilinganishwa na vichujio vingine vya kawaida, kinaweza kupakia na kutekeleza maelfu ya kanuni za uchujaji. Matumizi: Bofya kitufe cha kuwasha/kuzima kwenye dirisha ibukizi ili kuzima au kuwasha uchujaji kwa kudumu kwa ukurasa wa wavuti wa sasa katika uBlock₀. Kitufe hiki kinadhibiti uchujaji wa maombi ya ukurasa wa wavuti wa sasa pekee; si swichi ya kudhibiti uchujaji kwa ujumla. Kitufe hiki kinadhibiti uchujaji wa maombi ya ukurasa wa wavuti wa sasa pekee; si swichi ya kudhibiti uchujaji kwa ujumla. *** Ni zaidi ya kizuizi cha matangazo: kinaweza pia kusoma na kuunda kanuni za uchujaji kutoka kwenye faili za hosts. Orodha zifuatazo za vichujio hupakiwa na kutekelezwa kwa chaguomsingi: - Orodha za vichujio za uBO - EasyList - EasyPrivacy - Peter Lowe’s Ad server list - Online Malicious URL Blocklist Kuna orodha zaidi unazoweza kuchagua: - EasyList Cookie List - Fanboy's Annoyance List - AdGuard Annoyances - Faili ya hosts ya Dan Pollock - Na nyingine zaidi Tafadhali kumbuka pia kwamba kuchagua orodha za ziada kunaweza kuongeza uwezekano wa kurasa za wavuti kutofanya kazi vizuri, hasa orodha ambazo kwa kawaida hutumiwa kama faili za hosts. *** Bila orodha hizi za vichujio, kiendelezi hiki kisingekuwa na maana. Kwa hiyo, ikiwa kweli unataka kuchangia, wafikirie watu wanaotunza orodha za vichujio: wao ndio wanaowezesha kila mtu kutumia haya yote bila malipo. *** Bila malipo. Msimbo wake uko wazi chini ya leseni ya umma ya GPLv3. Kila kitu kwa ajili ya mtumiaji. Wachangiaji kwenye Github: https://github.com/gorhill/uBlock/graphs/contributors Wachangiaji kwenye Crowdin: https://crowdin.net/project/ublock *** Hili bado ni toleo lililo katika hatua za mwanzo kwa kiasi fulani, kwa hiyo tafadhali zingatia hilo unapolipitia na kutoa tathmini yako. Kumbukumbu ya mabadiliko ya mradi: https://github.com/gorhill/uBlock/releases