Picha za skrini

Maelezo

Furahia ulinzi zaidi wa kivinjari ukitumia ESET Browser Privacy & Security. Browser Privacy & Security ni kiendelezi cha kivinjari kilichoundwa kwa ajili ya viwango vya usajili wa ESET HOME Security. Hufanya kazi pamoja na teknolojia ya ESET iliyoshinda tuzo ili kuongeza safu nyingine ya ulinzi katika maisha yako ya kidijitali—ikitoa usalama na faragha zaidi kwenye kivinjari. Unaweza kukiwasha kwa urahisi kupitia kiwango chako cha ESET HOME Security, na kina kiolesura rahisi kutumia kinachorahisisha matumizi ya intaneti. Kinapatikana kwa Windows pekee. Utendaji unajumuisha: Utafutaji Salama – Tofautisha kwa urahisi matokeo salama ya utafutaji na yasiyo salama. Utendaji huu hukulinda dhidi ya tovuti zinazolenga kuiba taarifa kwa ulaghai, tovuti zenye programu hasidi, na maudhui yanayoweza kuwa yasiyotakikana. Usafishaji wa Kivinjari – Futa data ya kivinjari chako unapohitaji, au mara kwa mara kwa usafishaji wa kiotomatiki—ukipunguza mrundikano wa data za kidijitali na kuboresha ufanisi wa kivinjari. Utendaji huu huwawezesha watumiaji kubinafsisha usafishaji na kubaki wameingia kwenye tovuti wanazotumia mara kwa mara. Ukaguzi wa Mipangilio ya Tovuti – Kagua na udhibiti ruhusa za tovuti kwa urahisi, ili kuhakikisha zina ufikiaji unaofaa wa kifaa chako na taarifa zako binafsi.* Usafishaji wa Metadata – Shiriki picha na maudhui yako mengine ya midia kwa kujiamini. Utendaji huu wa kipekee hulinda faragha yako kwa kuondoa metadata kwenye picha zinazopakiwa kwenye kivinjari chako. Metadata ina taarifa kama vile GPS, aina ya kamera, na muda picha ilipopigwa—ambazo zinaweza kufichua taarifa binafsi. Kwa sasa inaauni faili za JPEG.* *Inapatikana kwa kiwango cha ESET HOME Security Ultimate pekee. Kwa maelezo ya kina kuhusu viwango vyetu vya usajili, tafadhali tembelea www.eset.com/int/home/protection-plans.