Picha za skrini

Maelezo

Ukiwa nyumbani, kazini, au safarini, Bitwarden hulinda kwa urahisi nywila zako zote, funguo za kuingia, na taarifa nyeti Imetambuliwa kuwa kidhibiti bora zaidi cha nywila na PCMag, WIRED, The Verge, CNET, G2, na wengine wengi! LINDA MAISHA YAKO YA KIDIJITALI Linda maisha yako ya kidijitali na ujikinge dhidi ya uvujaji wa data kwa kuzalisha na kuhifadhi nywila imara na za kipekee kwa kila akaunti. Weka kila kitu katika hifadhi ya nywila iliyosimbwa kwa njia fiche kutoka mwanzo hadi mwisho, ambayo ni wewe pekee unayeweza kuifikia. FIKIA DATA YAKO POPOTE, WAKATI WOWOTE, KWENYE KIFAA CHOCHOTE Dhibiti, hifadhi, linda, na ushiriki kwa urahisi idadi isiyo na kikomo ya nywila kwenye idadi isiyo na kikomo ya vifaa, bila vizuizi. KILA MTU ANAPASWA KUWA NA ZANA ZA KUKAA SALAMA MTANDAONI Tumia Bitwarden bila malipo, bila matangazo wala kuuzwa kwa data. Bitwarden inaamini kwamba kila mtu anapaswa kuwa na uwezo wa kukaa salama mtandaoni. Mipango ya Premium hutoa ufikiaji wa vipengele vya hali ya juu. ZIPATIE TIMU ZAKO UWEZO KWA BITWARDEN Mipango ya Teams na Enterprise ina vipengele vya kitaalamu vya biashara. Mifano ni pamoja na ujumuishaji wa SSO, kuendesha mfumo kwenye seva zako mwenyewe, ujumuishaji wa saraka na usanidi wa akaunti kupitia SCIM, sera zinazotumika katika shirika zima, ufikiaji wa API, kumbukumbu za matukio, na zaidi. Tumia Bitwarden kulinda wafanyakazi wako na kushiriki taarifa nyeti na wenzako kazini. Sababu zaidi za kuchagua Bitwarden: Usimbaji Fiche wa Kiwango cha Kimataifa Nywila zinalindwa kwa usimbaji fiche wa hali ya juu kutoka mwanzo hadi mwisho (AES-256 bit, uundaji wa hashi kwa kuongeza data nasibu, na PBKDF2 SHA-256) ili data yako ibaki salama na ya faragha. Ukaguzi wa Wataalamu Huru Bitwarden hufanya mara kwa mara ukaguzi wa kina wa usalama unaofanywa na kampuni huru mashuhuri za usalama. Ukaguzi huu wa kila mwaka unajumuisha tathmini za msimbo chanzo na majaribio ya kupenya mifumo katika anwani za IP, seva, na programu za wavuti za Bitwarden. Uthibitishaji wa Hatua Mbili (2FA) wa Hali ya Juu Linda kuingia kwako kwa kutumia programu ya uthibitishaji ya mtoa huduma mwingine, misimbo inayotumwa kwa barua pepe, au vitambulisho vya FIDO2 WebAuthn kama vile ufunguo wa usalama wa kifaa au ufunguo wa kuingia. Bitwarden Send Tuma data moja kwa moja kwa wengine huku ukidumisha usalama wa usimbaji fiche kutoka mwanzo hadi mwisho na kupunguza uwezekano wa data kufichuka. Kizalishaji Kilichojumuishwa Unda nywila ndefu, changamani, na tofauti, pamoja na majina ya watumiaji ya kipekee kwa kila tovuti unayotembelea. Unganisha na watoa huduma za anwani mbadala za barua pepe kwa faragha ya ziada. Tafsiri za Lugha Mbalimbali Duniani Bitwarden inapatikana katika tafsiri za lugha zaidi ya 60, zilizotafsiriwa na jumuiya ya kimataifa kupitia Crowdin. Programu za Mifumo Mbalimbali Linda na ushiriki data nyeti iliyo ndani ya Bitwarden Vault yako kutoka kwenye kivinjari chochote, kifaa cha mkononi, au mfumo wa uendeshaji wa kompyuta, na zaidi. Bitwarden hulinda zaidi ya nywila pekee Suluhisho za Bitwarden za kudhibiti vitambulisho vya kuingia kwa usimbaji fiche kutoka mwanzo hadi mwisho huwezesha mashirika kulinda kila kitu, ikiwemo taarifa za siri zinazotumiwa na wasanidi programu na matumizi ya funguo za kuingia. Tembelea Bitwarden.com ili kujifunza zaidi kuhusu Bitwarden Secrets Manager na Bitwarden Passwordless.dev!