True Key™ by McAfee
ID
cpaibbcbodhimfnjnakiidgbpiehfgciHifadhi na ujaze manenosiri kiotomatiki, sawazisha maelezo ya akaunti kwenye vifaa mbalimbali, na ulinde ufikiaji kwa vipengele vingi vya uthibitishaji.
Picha za skrini
Maelezo
Endelea tu, sahau manenosiri yako. Kwa programu ya True Key, wewe ndiye nenosiri.
Kutana na True Key™ by McAfee – njia rahisi na salama zaidi ya kufungua ulimwengu wako wa kidijitali.
Hakuna tena usumbufu wa kukumbuka manenosiri mengi – ingia kwa urahisi kwenye programu, tovuti na vifaa vyako ukitumia programu ya True Key.
Ufikiaji wa Haraka na Rahisi
Kuanzia unapofungua kivinjari chako, kiendelezi cha kivinjari cha True Key hukusaidia kufikia akaunti zako kwa urahisi.
• Hifadhi na ujaze maelezo ya manenosiri yako kiotomatiki
• Furahia ufikiaji rahisi wa programu, tovuti na vifaa vyako
Linda Utambulisho Wako
Programu ya True Key hukupa uhuru wa kuongeza tabaka nyingi za ulinzi kwa ajili ya kufikia wasifu wako wa True Key, ikijumuisha mambo kama:
• Uthibitishaji kwa kifaa cha pili – tumia kifaa cha mkononi kuthibitisha kuwa ni wewe
• Kifaa kinachoaminika – True Key hutambua vifaa ambavyo ni vyako
• Nenosiri lako kuu moja – halihifadhiwi kamwe na ni wewe tu unayelijua
Kadiri unavyoongeza vipengele zaidi, ndivyo ulinzi wa wasifu wako wa True Key utakavyoimarika.
Pakua programu ya True Key kwenye vifaa na vivinjari vyako vyote ili upate ufikiaji popote ulipo. Data yako husawazishwa kiotomatiki, kwa hivyo utakuwa na taarifa unazohitaji wakati unapozihitaji.
Pata maelezo zaidi kwenye www.truekey.com