Picha za skrini

Maelezo

Dhibiti vidakuzi vyako! Baada ya kufunga vichupo, futa kiotomatiki vidakuzi usivyotaka kuhifadhi. Unaweza kuweka orodha ya kuruhusu kwa vidakuzi unavyotaka kuhifadhi. Vipengele vikuu - Hufuta kiotomatiki data za tovuti kutoka kwenye vichupo vilivyofungwa - Inasaidia orodha ya kuhifadhi daima/orodha ya kuhifadhi kwa muda - Hamisha/ingiza kwa urahisi orodha yako ya kuhifadhi daima/kwa muda - Futa data za tovuti kwa kikoa - Inasaidia usafishaji wa mwenyewe kutoka kwenye dirisha ibukizi Matumizi Kiendelezi hiki hakisafishi data kiotomatiki hadi uwashe "Auto-clean". Hii inakupa nafasi ya kuongeza tovuti kwenye orodha ya kuhifadhi daima. 1. Ongeza tovuti ambazo unataka kuhifadhi data zake kwenye orodha ya kuhifadhi daima (bila kikomo cha muda) au orodha ya kuhifadhi kwa muda (hadi kivinjari kianzishwe upya) 2. Washa "Auto-clean" kwenye dirisha ibukizi au "Automatic cleaning" kwenye mipangilio 3. Tazama data hizo za tovuti zisizotumika zikipotea :) Unaweza kuzima arifa za usafishaji kupitia mipangilio. Kumbuka: Data za tovuti ni vidakuzi, IndexedDB, Localstorage, n.k. Uwezo wa kuzifuta unategemea API za kivinjari na jinsi kiendelezi kilivyotekelezwa. Ukiwa na tatizo lingine lolote, liripoti kwenye GitHub. Huenda tukalitatua. Kumbuka kuwa msaada huenda usipatikane kwa matoleo yaliyorekebishwa ya Mozilla Firefox na Google Chrome.