Picha za skrini

Maelezo

Hifadhi chochote kilicho kwenye wavuti kwenye OneNote. Kihifadhi kama kipande kwenye OneNote, kipange na ukihariri, kisha ukifikie kutoka kwenye kifaa chochote. Una shughuli nyingi. OneNote Web Clipper hukuwezesha kuhifadhi haraka ukurasa mzima wa wavuti au sehemu yake kwenye OneNote kwa matumizi ya baadaye. Hifadhi picha, PDF, video au alamisho yenye picha ya ukurasa. Zaidi ya yote, unaweza kuvifikia kutoka kwenye kompyuta, kompyuta kibao au simu yoyote – hata ukiwa nje ya mtandao. HIFADHI VIPANDE KWA NJIA YAKO - HAKUNA MSONGAMANO! Makala, mapishi au bidhaa zinaweza kuhifadhiwa kama vipande bila matangazo yote, vipengele vya kuvinjari na vitu vinavyovuruga usomaji. - Angazia maandishi, rekebisha fonti au ongeza dokezo kabla ya kuhifadhi kipande. - Hifadhi ukurasa mzima au sehemu kadhaa ulizochagua kwenye ukurasa. Uamuzi ni wako. UNACHOWEZA KUHIFADHI KAMA KIPANDE - Ukurasa mzima wa wavuti au sehemu yake - Faili za PDF – mtandaoni au kwenye kompyuta yako - Picha yoyote kwenye ukurasa wa wavuti - Video kutoka YouTube au Vimeo - Unda alamisho yenye picha ya ukurasa INAFAA SANA KWA - Safari - Biashara - Ununuzi - Mapishi - Utafiti - Habari - Msukumo wa mawazo BEBA PAMOJA NAWE - Chochote unachohifadhi kama kipande kwenye OneNote kitapatikana kwenye vifaa vyako vyote, hata ukiwa nje ya mtandao. - Tumia utafutaji wenye uwezo mkubwa wa OneNote kupata taarifa zako kwenye kifaa chochote. - Shiriki taarifa zako na wengine.