Picha za skrini

Maelezo

Pochi ya kripto inayoaminika zaidi duniani MetaMask ndiyo pochi ya kripto iliyo salama zaidi na yenye unyumbufu mkubwa zaidi duniani, inayoaminiwa na mamilioni ya watumiaji kununua, kuuza na kubadilisha mali za kidijitali. Dhibiti mkusanyiko wako wa uwekezaji, tumia programu zilizogatuliwa, na uingie kwenye wavuti iliyogatuliwa. Kripto imerahisishwa – Nunua, uza, badilisha na upate mapato moja kwa moja ndani ya pochi yako – Chagua kutoka maelfu ya tokeni – Unganisha kwenye programu zilizogatuliwa katika blockchain nyingi – Jaribu DeFi, nunua sarafu za meme, kusanya NFT, chunguza michezo ya web3, na zaidi Usalama wa hali ya juu unaoongoza katika sekta unakulinda – Fahamu unachosaini kabla ya kufanya muamala – Ufuatiliaji wa vitisho kwa wakati halisi unalinda pochi yako – Imeundwa kwa ajili ya faragha; dhibiti unachoshiriki – Ulinzi dhidi ya MEV na kuingizwa kwa miamala ya wengine mbele ya yako Usaidizi wa moja kwa moja saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki – Usaidizi saa zote kutoka kwa wataalamu wetu wa huduma kwa wateja (watu halisi!) MITANDAO INAYOTUMIKA Mitandao yote mikuu kama Ethereum, Bitcoin, Solana, BNB Chain na mingineyo. TOKENI ZINAZOTUMIKA BTC, ETH, USDT, SOL na mamia ya maelfu ya nyinginezo. Pakua MetaMask leo. Kwa kuwa MetaMask inaongeza utendaji kwenye kivinjari chako cha kawaida, tunahitaji ruhusa ya kusoma na kuandika kwenye ukurasa wowote wa wavuti. Unaweza kutazama msimbo wetu chanzo wakati wowote kama unavyofanya kwa kiendelezi chochote cha Chrome, au kwenye Github: https://github.com/MetaMask Sera yetu ya faragha: https://consensys.net/privacy-policy/ Masharti ya matumizi: https://consensys.net/terms-of-use/