Picha za skrini

Maelezo

Uchunguzi wa hisabati wenye mvuto, uwezo mkubwa na usiolipishwa! Unaletwa kwako na desmos.com Chunguza hisabati ukitumia Desmos! Chora grafu za fanksheni, unda majedwali, ongeza vitelezi, huisha grafu zako, na mengine mengi — yote bila malipo. Hapa Desmos, tunawazia ulimwengu ambamo kila mtu ana ujuzi wa msingi wa hisabati na ambamo hisabati inapatikana kwa urahisi na inafurahisha kwa wanafunzi wote. Tunaamini kuwa ufunguo ni kujifunza kwa kufanya. Ili kutimiza maono haya, tumeanza kwa kujenga kizazi kijacho cha kikokotoo cha grafu. Kwa kutumia mfumo wetu wa kukokotoa hisabati wenye uwezo mkubwa na kasi ya ajabu, kikokotoo kinaweza kuchora papo hapo grafu ya mlinganyo wowote, kuanzia mistari na parabola hadi viambajengo na mifululizo ya Fourier. Vitelezi hurahisisha kuonyesha mabadiliko ya fanksheni. Ni hisabati yenye mvuto na iliyo rahisi kuelewa. Na jambo bora zaidi: ni bure kabisa. Vipengele: Uchoraji wa grafu: Chora grafu za viwianishi vya pola, viwianishi vya Karteziani au grafu zinazobainishwa kwa vigezo. Hakuna kikomo cha idadi ya semi unazoweza kuchora grafu zake kwa wakati mmoja — wala huhitaji kuingiza semi katika umbo la y=! Vitelezi: Rekebisha thamani kwa kuingiliana nazo ili kukuza uelewa wa moja kwa moja, au huisha kigezo chochote ili kuona athari yake kwenye grafu Majedwali: Ingiza data na uichore kwenye grafu, au unda jedwali la thamani za ingizo na matokeo kwa fanksheni yoyote Takwimu: Tafuta mistari, parabola na mikunjo mingine inayolingana vizuri zaidi na data. Kukuza na kupunguza mwonekano: Badilisha vipimo vya mihimili kila mmoja peke yake au yote kwa wakati mmoja kwa kusogeza vidole viwili pamoja au kuvitenganisha, au rekebisha ukubwa wa dirisha mwenyewe ili kupata mwonekano unaofaa kabisa. Nukta muhimu: Gusa mkunjo ili kuonyesha nukta za thamani za juu zaidi, za chini zaidi na za makutano. Gusa nukta muhimu za kijivu ili kuona viwianishi vyake. Shikilia kidole kwenye mkunjo na ukiburute kuufuata ili kuona viwianishi vikibadilika chini ya kidole chako. Kikokotoo cha kisayansi: Andika tu mlinganyo wowote unaotaka kutatua na Desmos itakuonyesha jibu. Kinaweza kushughulikia mizizi ya pili, logaritimu, thamani za umbali wa namba kutoka sifuri na mengine mengi. Tosisawa: Chora grafu za tosisawa katika viwianishi vya Karteziani na vya pola. Tembelea www.desmos.com ili kujifunza zaidi.