WeDo 2.0 LEGO® Education
ID
pflionopdgpjckjkafnlamfmonjhccdhProgramu ya LEGO® Education WeDo 2.0 inawawezesha wanafunzi kuchunguza miradi mizuri ya sayansi.
Maelezo ya kiendelezi
Maelezo
Programu ya LEGO® Education WeDo 2.0 inawawezesha wanafunzi kuchunguza miradi mizuri ya sayansi.
Inaoana na Chromebook pekee!
WeDo 2.0 huwawezesha wanafunzi wa shule ya msingi kuandika msimbo. Kwa kutumia vipande vya LEGO®, programu rahisi kutumia na miradi ya STEM inayovutia, walimu wana kila wanachohitaji kuwafundisha wanafunzi wao ujuzi rahisi wa upangaji programu.
Mchanganyiko huu wa kipekee wa kujenga kwa vipande vya LEGO®, kisha kutumia programu rahisi ya darasani kuifanya WeDo 2.0 ianze kufanya kazi kupitia mipango ya masomo inayovutia ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati, hukupa kila unachohitaji kufundisha upangaji programu darasani.
NUKUU
“WeDo 2.0 inatoa miradi inayowaruhusu wanafunzi kugundua uso wa Mirihi kwa mfano wa gari la uchunguzi, au kuchunguza msitu wa mvua wa Amazon kupitia mabadiliko ya maumbile ya chura.” - JEFFREY MARLOW, mwanajiobiolojia katika Harvard University na mwanzilishi wa The Mars Academy Education and Development Program
“Kuna sababu kwa nini LEGO ni kifaa cha kuchezea kinachopendwa zaidi duniani. Mbali na kuhamasisha na kukuza ubunifu wa watoto, kinaweza pia kutumiwa kama zana muhimu ya kufundishia, kama zinavyoonyesha seti mpya za WeDo 2.0 za kampuni hiyo za roboti na uandishi wa msimbo.” – GIZMODO
“Suluhisho za LEGO® Education zinasaidia sana kuwashirikisha wanafunzi na kuwaandaa kwa chuo na kazi, ambalo ndilo lengo letu la mwisho.” - FREDERICK TUDDA, mkuu wa shule, P.S. 188, New York
TUZO
Teknolojia Bora kwa Wanaopenda Kutengeneza Vitu: LEGO® Education WeDo 2.0
“LEGO® Education WeDo 2.0 ni seti ya roboti kwa elimu inayowatambulisha watoto wa shule ya msingi kwenye ulimwengu wa upangaji programu. Kwa kutumia roboti inayovutia na programu inayoambatana nayo, wanafunzi wa darasa la 2 hadi la 4 wanaweza kuelewa jinsi msimbo unavyoundwa. Bidhaa hii pia imeundwa kwa ajili ya waelimishaji, ambao wanaweza kutumia mtaala ulioambatanishwa kufundisha misingi ya sayansi. Bidhaa hii ilishinda si kwa ubunifu wake kama seti ya zana za elimu pekee, bali pia kwa bei yake nafuu.” – MONA LALWANI, mhariri mwandamizi, ___________
• Golden Product Award ya 2017 kutoka CEEIA (China Educational Equipment Industry Association)
• Parent Award 2016
• Best of CES 2016
• Gotta Be Mobile Excellence Award 2016
• Worlddidac Award 2016
• New York Design Awards
• TOMMI German Children Software Award
Kwa programu ya shule ya WeDo 2.0 na seti ya vipande vya LEGO®, unaweza:
- Kuimarisha uelewa wa wanafunzi wa mbinu 8 za sayansi na uhandisi, zikiwemo kuuliza maswali na kutatua matatizo, kutengeneza miundo, kutengeneza vielelezo vya awali, kufanya uchunguzi, kuchanganua na kutafsiri data, kufikiri kwa njia ya kimahesabu ya kompyuta, kujenga hoja zinazotegemea ushahidi na kupata, kutathmini na kuwasilisha taarifa.
- Kukuza umahiri kupitia mipango ya masomo ya vitendo kuhusu mada muhimu za sayansi kama sayansi za fizikia, sayansi za uhai, sayansi za dunia na anga, na uhandisi, teknolojia na matumizi ya sayansi.
- Kuboresha ujuzi wa wanafunzi wako wa kutatua matatizo, kufikiri kwa makini, kuwasiliana na kushirikiana.
- Kujumuisha matumizi ya programu zinazofaa za elimu ili kuboresha ujuzi wa kufikiri kwa njia ya kimahesabu ya kompyuta.
- Suluhisho hili la programu kwa shughuli za vitendo darasani huchochea hamu ya asili ya wanafunzi ya kuchunguza na kugundua upangaji programu za kompyuta, na kwa kweli ndiyo njia bora zaidi ya kujifunza.
- Kuwafundisha watoto kuandika msimbo kwa programu ya elimu bora zaidi katika kundi lake, inayojumuisha mipango ya masomo ya zaidi ya saa 40 iliyotengenezwa kwa msingi wa Next Generation Science Standards.
*** MUHIMU***
Hii si programu ya elimu inayotumiwa peke yake. Programu hii hutumiwa kupanga utendaji wa seti ya vipande vya LEGO® Education WeDo 2.0, ambayo inauzwa kando. Tafadhali wasiliana na muuzaji wa LEGO Education wa eneo lako kwa maelezo zaidi.
Kuanza: www.legoeducation.com/start
Mipango ya Masomo: www.legoeducation.com/lessons
Usaidizi: www.lego.com/service
Twitter: www.twitter.com/lego_education
Facebook: www.facebook.com/LEGOeducationNorthAmerica
Instagram: www.instagram.com/legoeducation
LEGO na nembo ya LEGO ni alama za biashara na/au kazi zinazolindwa na hakimiliki za LEGO Group. ©2017 The LEGO Group. Haki zote zimehifadhiwa.