Picha za skrini

Maelezo

Tazama jinsi watu wanavyoingiliana na tovuti yako, moja kwa moja kutoka kwenye tovuti yako. Kiendelezi cha Microsoft Clarity Live hukusaidia kuona kwa urahisi maeneo ambayo watumiaji wanaingiliana na tovuti yako, wanapokwama, na kujaribu mawazo mapya. Pia huhitaji kwenda kwenye tovuti tofauti au kuchambua safu wima za data ili kupata taarifa unazohitaji. Clarity Live hukufanyia kazi ngumu kwa kutengeneza ramani za joto na rekodi za vipindi vya matumizi unazoweza kutazama bila kuondoka kwenye tovuti yako. Maonyesho haya ya data kwa njia ya picha hurahisisha uchanganuzi wa mwingiliano, uboreshaji wa muundo, na utambuzi na utatuzi wa matatizo kwa haraka. Jinsi inavyofanya kazi: Pakua kiendelezi na ufungue akaunti ya bure ya Clarity ikiwa bado huna. Kisha nenda tu kwenye ukurasa au hali mahususi ya matumizi unayotaka kuchunguza na uchague ikoni ya ramani ya joto, ramani ya joto ya eneo, au rekodi ya kipindi cha matumizi kwenye wijeti ya Clarity. Tayari! Kipengele chochote cha Clarity ulichochagua hufunguka moja kwa moja juu ya ukurasa uliopo. Ni hivyo tu. Uchanganuzi haujawahi kuwa rahisi hivi! Vipengele muhimu Ramani za joto: Clarity Live huunganisha aina mbili za ramani za joto katika mwonekano mmoja. Ramani za joto za mibofyo hurekodi vipengee vinavyobofwa zaidi (au kuguswa zaidi) kwenye ukurasa. Ramani za joto za kusogeza ukurasa hufichua maeneo yanayotazamwa zaidi kwenye ukurasa kwa kuonyesha watumiaji husogeza hadi wapi. Clarity Live hurahisisha kuona mwingiliano kwenye paneli zinazojitokeza, madirisha ibukizi, orodha kunjuzi na vipengee vingine ambavyo vinaweza kuwa vigumu kurekodi katika ramani za joto za kawaida. Ramani za joto za maeneo: Badala ya kuonyesha mwingiliano kwa kila kipengee, ramani hizi hukuruhusu kuchagua eneo linaloweza kuwa na vipengee kadhaa ili kupata jumla ya mibofyo na asilimia za mgawanyo wa mibofyo hiyo. Eneo linaweza kuwa na kipengee kimoja tu au kuwa kubwa kama ukurasa mzima. Wewe ndiye unayeamua. Rekodi za vipindi vya matumizi: Hizi hukuwezesha kutazama kwa karibu kila kipindi cha matumizi. Maonyesho haya yanayosogea hurekodi jinsi mtumiaji alivyochunguza tovuti yako, kwa kuonyesha alipobofya au kugusa, aliposita, na jinsi alivyosogeza kishale. Clarity Live pia hurahisisha sana kupata rekodi za hali mahususi ya matumizi. Kwa mfano, ikiwa ungetaka kuona jinsi mtumiaji anavyoingiliana na dirisha fulani ibukizi, ungeweza kufungua dirisha hilo kwenye tovuti yako na kuchagua ikoni ya kurekodi kwenye wijeti. Ungeona mara moja rekodi husika zilizofanywa ndani ya siku tatu zilizopita. Dokezo kuhusu bei: Clarity ni ya bure kwa 100%. Hutawahi kuombwa kubadili kwenda kwenye toleo la kulipia. Kadi ya mkopo haihitajiki kusajili akaunti ya Clarity. Pata maelezo zaidi(https://clarity.microsoft.com/pricing) Acha kubahatisha. Pata Clarity. Furahia kutazama data kwa njia ya picha!