Picha za skrini

Maelezo

Kiendelezi cha Chrome Remote Desktop Hiki ni kiendelezi kinachoambatana na tovuti ya Chrome Remote Desktop (https://remotedesktop.google.com). Kiendelezi hiki hukuwezesha kusakinisha, kuona na kurekebisha programu ya mteja ya Chrome Remote Desktop inayosakinishwa kwenye kifaa kupitia kiolesura cha wavuti. Chrome Remote Desktop huwawezesha watumiaji kufikia kompyuta nyingine wakiwa mbali kupitia kivinjari cha Chrome au Chromebook. Kompyuta zinaweza kuwekwa zipatikane kwa muda mfupi, kwa mfano kwa usaidizi wa mbali unaotolewa inapohitajika, au kwa muda mrefu zaidi ili kufikia programu na faili zako ukiwa mbali. Miunganisho yote imelindwa kikamilifu. Chrome Remote Desktop inafanya kazi kikamilifu kati ya mifumo tofauti. Toa usaidizi wa mbali kwa watumiaji wa Windows, Mac na Linux, au fikia maeneo-kazi yako ya Windows na Mac wakati wowote, yote kupitia kivinjari cha Chrome kwenye karibu kifaa chochote, zikiwemo Chromebook. Kwa maelezo kuhusu faragha, tafadhali angalia Sera ya Faragha ya Google na Ilani ya Faragha ya Chrome. Kwa usaidizi au utatuzi wa matatizo, tafadhali bofya hapa: https://support.google.com/chrome/answer/1649523