Exodus Web3 Wallet
ID
aholpfdialjgjfhomihkjbmgjidlcdnoDhibiti sarafu za kidijitali na NFT katika pochi ya Web3 ambayo funguo zake unazihifadhi mwenyewe, unganisha na programu, badilisha mali na weka sarafu za kidijitali kwenye staking.
Maelezo ya kiendelezi
Picha za skrini
Maelezo
Exodus inaunganisha Web3 kwa kutoa usaidizi bora zaidi wa minyororo mingi ya bloku bila kuchukua uhifadhi wa mali zako—kuanzia Solana hadi Ethereum na mingine zaidi.
Unganisha na programu za Web3 kwenye mitandao mingi kwa pochi moja, na mitandao zaidi ya Web3 inaendelea kuja.
Exodus inasaidia mitandao maarufu zaidi ya Web3 kama Ethereum, Solana na Cardano.
Pochi ya Web3 yenye uhifadhi unaodhibitiwa nawe
Jitose bila hofu katika Web3 na uchunguze ulimwengu wa DeFi, NFT na mengine mengi ukiwa na usalama na faragha za Exodus Web3 Wallet. Unadhibiti sarafu zako za kidijitali kikamilifu kwa sababu wewe, na wewe pekee, ndiye unayeshikilia funguo za faragha.
Nunua na uuze sarafu za kidijitali
Nunua sarafu za kidijitali kwa kadi yako ya mkopo/debiti, akaunti ya benki, Apple Pay au Google Pay, na ubadilike kwa urahisi kutoka pesa hadi sarafu za kidijitali. Uza sarafu za kidijitali upate pesa za kawaida na utoe fedha zako kwenda kwenye akaunti yako ya benki.
Badilisha sarafu za kidijitali
Tafuta kiotomatiki katika masoko mengi ya kubadilisha yasiyo na msimamizi mkuu (DEX) na upate bei bora zaidi ya kubadilisha sarafu zako za kidijitali kwenye mnyororo wa bloku. Fikia aina nyingi za tokeni kwa viwango vya chini zaidi vya ubadilishaji na kupitia njia za haraka zaidi kwa mibofyo michache tu. Badilisha mali maarufu zaidi kati ya minyororo ya bloku.
Pata zawadi za sarafu za kidijitali
Pata mapato yanayozalishwa bila kufanya kazi moja kwa moja, katika mfumo wa faida ya sarafu za kidijitali, kwa kuweka sarafu zako kwenye staking. Weka Solano na Cardano kwenye staking moja kwa moja katika programu, au unganisha pochi yako ya Exodus na programu za DeFi.
Ingiza kifungu cha kurejesha pochi
Tayari una pochi? Ingiza kifungu chako cha kurejesha kutoka kwenye pochi nyingine kama Phantom na MetaMask ili ufurahie Web3 kwa namna ya Exodus—salama na yenye mvuto.
Pochi yako ya NFT
Gundua mikusanyiko ya NFT inayovuma zaidi na udhibiti vitu vyako vya kidijitali vya kukusanya katika galeria yako mwenyewe ya NFT inayohusisha minyororo mingi ya bloku.
Msaada kutoka kwa watu saa 24 kila siku
Katika safari zako zote za Web3, uwe na uhakika kwamba tuko upande wako tukikupa huduma bora zaidi kwa wateja wakati wowote unapozihitaji.